top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kikokotoo: Kipimo cha mimba kwa mkojo baada ya Mimba kutoka

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Weka tarehe mimba ilipotoka na tarehe ya tendo la mwisho bila kinga, bonyeza 'Kokotoa'. Kipimo chanya zaidi ya wiki 4 hadi 6 baadaye – mwone mtoa huduma. Soma Kipimo chanya baada ya kusafishwa kizazi.



Maelezo


Jinsi ya kutumia


  • Weka tarehe mimba ilipotoka au kusafishwa.

  • Weka umri wa mimba ilipotoka (wiki).

  • Weka tarehe ya tendo la mwisho bila kinga (kama lipo).

  • Bonyeza 'Kokotoa' – utaona kama ni mapema kupima au kama majibu yanaweza kuaminika.


Kutafsiri


  • Chanya ndani ya wiki 2 hadi 4 – mara nyingi hCG iliyobaki.

  • Chanya baada ya wiki 4 hadi 6 – mabaki, mimba mpya au mimba zabibu; hCG ya damu na ultrasound.

  • Hasi – hCG imeshuka; mimba mpya kutoka tendo la karibuni haitaonekana mapema – pima wiki 3 baada ya tendo.

  • Soma Kutafsiri kipimo cha mimba.


Nini cha kufanya



Dalili za hatari


  • Damu nyingi, homa, maumivu makali, kizunguzungu – hospitali mara moja.


Lini umwone daktari



Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. hCG hukaa muda gani baada ya mimba kutoka?

Kwa kawaida wiki 2 hadi 4, wakati mwingine hadi wiki 6.

2. Kipimo chanya wiki 2 baadaye ni mimba mpya?

Mara nyingi ni hCG iliyobaki.

3. Kipimo chanya wiki 6 baadaye?

Mwone mtoa huduma – mabaki, mimba mpya au mimba zabibu.

4. Kikokotoo kinathibitisha mimba?

Hapana, ni mwongozo tu.

5. Naweza kushika mimba haraka baada ya mimba kutoka?

Ndiyo, kuanzia wiki 2.

6. hCG ya damu inasaidia?

Ndiyo, ikipimwa mara 2 hutofautisha kushuka na kupanda.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:17

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Schreiber CA, et al. Low serum human chorionic gonadotropin levels after medication abortion: a systematic review. Contraception. 2019;99(2):77–83.

  2. World Health Organization. Abortion care guideline. Geneva: WHO; 2022.

bottom of page