Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kuoga baada ya Kujifungua kwa Upasuaji: Mwongozo Kamili
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Shower ya uvuguvugu baada ya saa 24; usisugue mshono; kausha kwa kugusagusa. Hakuna beseni hadi mshono upone. Mshono mwekundu, unavimba, usaha au kufunguka – kituoni. Soma Kidonda cha upasuaji kutoa usaha.
Maelezo
Wakati
Saa 24 – shower/kumwaga maji, kwa ruhusa ya bandeji.
Siku chache – kuendelea kila siku.
Wiki 2–6 – beseni au kuogelea baada ya mshono kupona.
Hatua
Nawa mikono; vitu vyote karibu.
Maji ya uvuguvugu.
Sabuni laini isiyo na manukato; suuza vizuri.
Usisugue mshono; maji yatiririke tu.
Kausha kwa kugusagusa; acha hewa kidogo.
Vaa nguo safi, nyepesi zisizobana mshono.
Epuka
Maji ya moto sana – kizunguzungu, mishipa kupanuka.
Kuweka mafuta, poda au dawa za asili kwenye mshono.
Kuoga peke yako ukiwa na kizunguzungu.
Nini cha kufanya
Tembea mapema; maji ya kutosha.
Mkanda kwa faraja – soma Mkanda baada ya upasuaji.
Kujikanda kwa uvuguvugu mbali na mshono – soma Kujikanda baada ya upasuaji.
Lokia – soma Lokia baada ya upasuaji.
Dalili za hatari
Hospitali mara moja ukiwa na:
Homa, mshono kuvimba, kuwa mwekundu, usaha au kufunguka.
Damu nyingi ukeni.
Mguu mmoja kuvimba, kubanwa pumzi.
Kuzimia bafuni.
Lini umwone daktari
Mshono kuwasha sana au vipele.
Maumivu ya mshono yanayoongezeka badala ya kupungua.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Naoga lini baada ya upasuaji?
Shower baada ya saa 24, kwa maelekezo ya bandeji.
2. Maji yataumiza mshono?
Hapana yakitiririka bila kusugua.
3. Beseni lini?
Baada ya mshono kupona, wiki 2–6.
4. Maji ya chumvi kwenye mshono?
Si lazima; maji safi yanatosha.
5. Nikiwa na kizunguzungu?
Kaa kwenye kiti; mtu awe karibu.
6. Mafuta kwenye mshono?
Hapana hadi upone.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:21
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
National Institute for Health and Care Excellence. Caesarean birth (NG192). London: NICE; 2021.
World Health Organization. WHO recommendations on maternal and newborn care for a positive postnatal experience. Geneva: WHO; 2022.
Toon CD, et al. Early versus delayed post-operative bathing or showering to prevent wound complications. Cochrane Database Syst Rev. 2015;(7):CD010075.

