Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt Peter A, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kushindwa kunyonya, homa, mwili kulegea
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Mpeleke hospitali sasa hivi. Njiani mweke kifuani mwako (ngozi kwa ngozi) apate joto, na jaribu kumnyonyesha kama anaweza kumeza.
Maelezo
Dalili za hatari kwa mtoto mchanga (WHO)
Hanyonyi au ananyonya vibaya.
Degedege.
Kupumua haraka (pumzi 60 au zaidi kwa dakika) au kifua kuingia ndani anapovuta pumzi.
Joto 37.5°C au zaidi, au chini ya 35.5°C (mwili baridi).
Hasogei, au anasogea tu akiguswa – mwili kulegea.
Manjano ndani ya saa 24 za kwanza, au viganja na nyayo kuwa njano.
Kitovu chekundu chenye usaha au harufu.
Visababishi vya mara kwa mara
Maambukizi kutoka kwa mama wakati wa kujifungua – soma Maambukizi kwa mtoto mchanga.
Homa ya uti wa mgongo, nimonia.
Sukari kushuka, mwili kupoa (hasa watoto njiti).
Nini cha kufanya
Usimpe dawa za homa wala za kienyeji kabla ya kumwona mtoa huduma.
Usimfunike sana mwenye homa; mwenye baridi – ngozi kwa ngozi na kofia.
Beba kadi ya kliniki ya mtoto.
Baadaye – nyonyesha mara nyingi; soma Namna nzuri ya kunyonyesha.
Nawa mikono kabla ya kumshika mtoto; tunza kitovu kikavu.
Dalili za hatari
Hospitali MARA MOJA ukiona dalili yoyote kati ya hizi:
Hanyonyi, analegea, homa au mwili baridi.
Degedege, kupumua haraka, midomo kuwa ya bluu.
Utosi kuvimba.
Kutapika kila kitu au matapishi ya kijani.
Lini umwone daktari
Ananyonya kidogo kuliko kawaida.
Hakojoi angalau mara 6 kwa siku.
Manjano yanaongezeka.
Kitovu chekundu kuzunguka.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Mtoto mchanga hanyonyi na ana homa, nifanyeje?
Hospitali mara moja; ni dalili ya hatari.
2. Mtoto mchanga ana mwili baridi, ni hatari?
Ndiyo; mweke ngozi kwa ngozi na nenda hospitali.
3. Nimpe paracetamol kwanza?
Hapana, nenda hospitali kwanza.
4. Mtoto analala tu haamki kunyonya, ni kawaida?
Hapana, kulegea ni dalili ya hatari.
5. Homa kwa mtoto mchanga ni nyuzi ngapi?
37.5°C au zaidi; chini ya 35.5°C pia ni hatari.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.
World Health Organization. Integrated Management of Childhood Illness: management of the sick young infant aged up to 2 months. Geneva: WHO; 2019.
World Health Organization. WHO recommendations on maternal and newborn care for a positive postnatal experience. Geneva: WHO; 2022.

