top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Glory, MD

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kusinyaa ngozi

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Kama unatumia krimu ya kujichubua au yenye steroid, iache taratibu kwa ushauri na mwone mtoa huduma wa ngozi. Soma Mabaka usoni.


Maelezo


Dalili


  • Ngozi nyembamba, inayong'aa, mikunjo midogo kama karatasi.

  • Mishipa midogo ya damu kuonekana – soma Michirizi ya mishipa ya damu kwenye ngozi.

  • Michirizi ya zambarau au nyeupe (stretch marks).

  • Kuchubuka na kupata vidonda kwa urahisi, kupona polepole.

  • Rangi kupotea au madoa; ngozi kavu – soma Kukauka kwa ngozi.


Visababishi


  • Krimu zenye steroid (clobetasol, betamethasone na nyingine), hasa usoni, kwenye mikunjo, au kwa ajili ya kujichubua.

  • Sindano za steroid kwenye ngozi au jointi – kibonyeo mahali palipodungwa.

  • Uzee na jua – kolajeni hupungua.

  • Magonjwa – lupus, scleroderma, lichen sclerosus (sehemu za siri), kisukari.

  • Steroid za kumeza muda mrefu.


Nini cha kufanya


  • Usitumie krimu ya steroid bila maelekezo; isitumike usoni zaidi ya muda ulioandikiwa.

  • Ukitumia muda mrefu, usiache ghafla – mtoa huduma atapunguza taratibu; ngozi inaweza kuwaka kwa muda.

  • Paka mafuta ya kulainisha ngozi kila siku.

  • Jikinge na jua – kofia, mavazi, krimu ya kujikinga na jua.

  • Usinunue krimu za kujichubua – nyingi zina steroid au zebaki.

  • Krimu ya steroid juu ya fangasi huzisambaza zaidi – soma Fangasi zinazoenea mwilini.


Dalili za hatari


  • Vidonda visivyopona, usaha au homa.

  • Ngozi kuwa ngumu na kubana ghafla, vidole kubadilika rangi kwenye baridi.

  • Uso wa mviringo, kuongezeka uzito, presha juu baada ya steroid nyingi.


Lini umwone daktari


  • Ngozi nyembamba au michirizi baada ya krimu.

  • Madoa meupe yanayowasha sehemu za siri.

  • Mabadiliko ya ngozi pamoja na maumivu ya jointi au vidonda mdomoni.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Krimu ya kujichubua inaweza kusinyaza ngozi?

Ndiyo, nyingi zina steroid zinazopunguza unene wa ngozi.

2. Ngozi iliyosinyaa inarudi kawaida?

Kidogo ukiacha mapema; michirizi hubaki.

3. Naweza kuacha krimu ya steroid ghafla?

Kama umetumia muda mrefu, punguza taratibu kwa ushauri.

4. Mishipa midogo usoni inatokana na nini?

Mara nyingi steroid, jua au umri.

5. Mafuta gani yanasaidia ngozi iliyosinyaa?

Ya kulainisha yasiyo na harufu, na kinga ya jua.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:08:33

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Hengge UR, et al. Adverse effects of topical glucocorticosteroids. J Am Acad Dermatol. 2006;54(1):1–15.

  2. World Health Organization. Mercury in skin lightening products. Geneva: WHO; 2019.

  3. Barnes L, et al. Reducing the risk of skin atrophy from topical corticosteroids. Br J Dermatol. 2021;185(4):698–709.

bottom of page