top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkk. Mangwella S, MD

Dkt. Sospeter B, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:43

Majira na magonjwa ya moyo

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Ugonjwa wa moyo au vihatarishi vingi – epuka vidonge vyenye estrojeni na sindano ya Depo. Chagua kitanzi cha shaba, au projestini pekee (vidonge, kipandikizi, kitanzi cha homoni) baada ya ushauri. Soma Nani hapaswi kutumia vidonge vya majira.


Maelezo


Kulingana na WHO (MEC)


  • Ugonjwa wa mishipa ya moyo au kiharusi: vidonge vya vichocheo viwili – usitumie; Depo – haishauriwi; projestini pekee na kipandikizi – huweza kuanza kwa uangalizi; kitanzi cha shaba – salama.

  • Vihatarishi vingi kwa pamoja (umri ≥35, sigara, presha, kisukari, mafuta mengi damuni): vidonge vya vichocheo viwili – usitumie au kwa tahadhari kubwa; Depo – haishauriwi.

  • Ugonjwa wa valvu wenye matatizo (presha ya mapafu, mpapatiko wa moyo, historia ya endokadaitisi): vidonge vya vichocheo viwili – usitumie.


Kwa nini


  • Estrojeni huongeza uwezekano wa damu kuganda.

  • Depo hupunguza mafuta mazuri (HDL) na athari zake hudumu miezi kadhaa baada ya sindano.


Nini cha kufanya


  • Mwambie mtoa huduma historia yako yote ya moyo, presha, kisukari na sigara.

  • Pima presha kabla ya kuanza njia yoyote ya homoni.

  • Acha kuvuta sigara.

  • Soma: presha, kiharusi, sigara, kisukari.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja ukiwa unatumia majira na una:


  • Maumivu makali ya kifua au kushindwa kupumua.

  • Mguu mmoja kuvimba na kuuma.

  • Upande mmoja wa mwili kulegea, kushindwa kuongea, au uono kupotea ghafla.

  • Kichwa kuuma sana ghafla.


Lini umwone daktari



Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Nina ugonjwa wa moyo, naweza kutumia vidonge vya majira?

Vyenye estrojeni hapana; projestini pekee huweza, baada ya ushauri.

2. Njia ipi ni salama zaidi?

Kitanzi cha shaba.

3. Sindano ya Depo inafaa?

Haishauriwi kwa mwenye ugonjwa wa moyo au vihatarishi vingi.

4. Kipandikizi (implant) kinafaa?

Kwa kawaida ndiyo, baada ya kuchunguzwa.

5. Navuta sigara na nina miaka 38, nitumie vidonge?

Hapana kwa vyenye estrojeni; chagua njia nyingine.

6. Dalili gani za hatari nikiwa natumia majira?

Maumivu ya kifua, mguu kuvimba, kulegea upande mmoja, kichwa kuuma ghafla.

7. Mimba yenyewe ni hatari kwa mwenye moyo dhaifu?

Huweza kuwa hatari – ndiyo maana njia madhubuti ya uzazi wa mpango ni muhimu.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:10

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. World Health Organization. Medical eligibility criteria for contraceptive use. 5th ed. Geneva: WHO; 2015.

  2. Roos-Hesselink JW, Cornette J, Sliwa K, et al. Contraception and cardiovascular disease. Eur Heart J. 2015;36(27):1728–34.

  3. Curtis KM, et al. U.S. Medical Eligibility Criteria for Contraceptive Use, 2024. MMWR Recomm Rep. 2024;73(4):1–126.

bottom of page