Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
2 Aprili 2026, 16:07:13

Majira na uzito
Hapana!
Wanawake walio wengi hawaongezeki au kupungua uzito kutokana na matumizi ya vidonge vya majira yenye vichocheo viwili.
Kwa kawaida uzito hubadilika hali ya maisha inapobadilika na watu wanapoongezeka umri. Kwa sababu mabadiliko haya ya uzito ni ya kawaida, wanawake wengi wanafikiri kuwa vidonge hivi husababisha kuongezeka au kupungua kwa uzito.
Je ni wanawake wote huwa hawaongezeki uzito
Hapana!
Wanawake wachache hupata mabadiliko ya ghafla ya uzito wakitumia vidonge vyenye vichocheo viwili. Mabadiliko haya hubadilika wakiacha kutumia vidonge hivi. Haijulikani ni kwa nini wanawake hawa wanapata mabadiliko ya uzito wanapotumia vidonge vya majira vyenye vichocheo viwili.
Soma zaidikuhusu majira na mabadiliko ya uzito kwenye makala ya Vidonge vya majira na uzito.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:07:13
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
