Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
2 Aprili 2026, 16:07:19

Matumizi ya neuroton kwa mtu mzima
Dawa Neuroton ni kirutubisho cha lishe ambacho mara nyingi hutumika kusaidia afya ya mishipa ya fahamu. Inapatikana kama tembe na mara nyingi hujumuisha mchanganyiko wa vitamini B.
Viambato vya Neuroton
Kwa kawaida neuroton huwa na mchanganyiko wa;
Vitamin B1 (Thiamine)
Vitamin B6 (Pyridoxine)
Vitamin B12 (Cyanocobalamin)
Matumizi ya Neuroton kwa mtu mzima
Matatizo ya neva (Magonjwa ya neva): Kama vile hisia za ganzi, kuchomachoma, na udhaifu wa neva – hasa kwa wagonjwa wa kisukari, shinikizo la damu au baada ya majeraha.
Upungufu wa vitamini B1, B6, na B12: Hasa kwa watu wenye lishe duni, wazee, au waliotumia pombe kwa muda mrefu.
Maumivu ya neva: Kama vile maumivu ya mgongo, shingo au miguu yenye asili ya neva.
Kuchoka kwa mwili na akili: Husaidia kuboresha utendaji wa neva na kuongeza nishati mwilini.
Dozi kwa mtu mzima
Kwa kawaida: Kidonge 1 mara 1 hadi 3 kwa siku, baada ya chakula (kulingana na ushauri wa daktari). Dozi inaweza kutofautiana kulingana na hali ya mgonjwa na maagizo ya daktari.
Tahadhari
Usitumie dozi kubwa bila ushauri wa daktari.
Overdose ya vitamin B6 kwa muda mrefu inaweza kusababisha madhara kwenye neva.
Mjamzito au mama anayenyonyesha anatakiwa kushauriana na daktari kabla ya kutumia.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:07:19
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
