Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. SAlome A, MD
Dkt. Benjamin L, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Mlo wa kutibu pumu ya ngozi
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Tiba kuu ni kulainisha ngozi kila siku na dawa za kupaka za mwongozo. Usiache vyakula bila vipimo vya mzio. Soma Pumu ya ngozi au ukurutu.
Maelezo
Ushahidi kuhusu vyakula
Mlo wa kuondoa vyakula – husaidia tu kwa mzio uliothibitishwa.
Mlo wa kupunguza michomo/Mediterania – mzuri kwa afya; faida maalumu kwa ukurutu bado inahitaji tafiti zaidi.
Mafuta ya samaki, vitamin D, probiotiki – tafiti ndogo zimeonyesha faida kidogo kwa baadhi; tafiti kubwa zinahitajika.
Ayurveda, usio na gluten – bado hakuna tafiti za kutosha (isipokuwa kwa wenye ugonjwa wa celiac).
Tiba yenye ushahidi
Mafuta mazito yasiyo na harufu (emollient) mara 2 kwa siku na baada ya kuoga.
Dawa ya steroid ya kupaka kwa vipindi vifupi, kwa maelekezo.
Kuepuka sabuni kali, maji ya moto sana, nguo za sufu.
Kutibu maambukizi ya ngozi mapema.
Nini cha kufanya
Andika chakula na dalili kama unashuku chakula fulani – kisha mwone mtoa huduma.
Mtoto: usiondoe maziwa au mayai bila ushauri.
Kunyonyesha hulinda watoto wachanga.
Kucha fupi; usikune.
Dalili za hatari
Hospitali mara moja ukiwa na:
Midomo, ulimi au uso kuvimba na kupumua kwa shida baada ya chakula.
Malengelenge mengi yenye maumivu na homa (maambukizi ya malengelenge juu ya ukurutu).
Lini umwone daktari
Ukurutu haupungui kwa mafuta na dawa za kawaida.
Mtoto hakui vizuri au anapangiwa mlo wa kuacha vyakula vingi.
Ngozi ina usaha au ganda la njano.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Kuna mlo unaotibu ukurutu?
Hapana; mlo bora husaidia afya, si tiba.
2. Niache maziwa?
Tu kama mzio umethibitishwa.
3. Mafuta ya samaki yanasaidia?
Tafiti ndogo zimeonyesha faida kidogo; tafiti kubwa zinahitajika.
4. Mlo usio na gluten unafaa?
Bado hakuna tafiti za kutosha kwa ukurutu.
5. Tiba kuu ni ipi?
Kulainisha ngozi kila siku na dawa za kupaka za mwongozo.
6. Chakula kinaweza kuamsha ukurutu?
Kwa wachache wenye mzio, ndiyo.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:50
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Bath-Hextall FJ, Delamere FM, Williams HC. Dietary exclusions for established atopic eczema. Cochrane Database Syst Rev. 2008;(1):CD005203.
Bath-Hextall FJ, et al. Dietary supplements for established atopic eczema. Cochrane Database Syst Rev. 2012;(2):CD005205.
National Institute for Health and Care Excellence. Atopic eczema in under 12s: diagnosis and management (CG57). London: NICE; 2007 (updated 2023).
Wollenberg A, et al. European guideline (EuroGuiDerm) on atopic eczema. J Eur Acad Dermatol Venereol. 2022;36(9):1409–31.

