top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

24 Agosti 2026, 03:43:15

Mtoto kutocheza tumboni kwa wakati

Swali la Mteja:

“Habari Daktari, mke wangu ametimiza wiki ya 21 ya ujauzito akiwa na mtoto wa pili lakini bado hajahisi mtoto kucheza. Je, kuna tatizo?”

Majibu ya kitaalamu

Katika ujauzito wa pili, akina mama wengi huanza kuhisi mtoto kucheza mapema zaidi, kuanzia wiki ya 16 hadi 20. Hata hivyo, si wanawake wote hupata hisia hizi mapema. Kuna baadhi ya wajawazito wanaweza kuchelewa kuzihisi, hasa kama:

  • Placenta ipo mbele ya tumbo (anterior placenta), hali inayozuia hisia mapema.

  • Mama hajui vyema kutofautisha hisia za gesi tumboni na zile za mtoto kucheza.

  • Mtoto yupo hai na anasogea, lakini kwa nguvu ndogo zisizohisiwa kwa sasa.


Tahadhari muhimu

Iwapo mama amefikisha wiki 21 na hajahisi kabisa harakati za mtoto, ni vyema kufanya uchunguzi wa ultrasound ili kuhakikisha kuwa mtoto anakua vizuri, ana mapigo ya moyo ya kawaida, na yupo hai.


Ushauri

  • Usiwe na hofu mapema ikiwa hakuna dalili nyingine za hatari kama maumivu makali au kutoka damu.

  • Fanya ultrasound kwa daktari au mtaalamu wa afya kwa uhakika wa maendeleo ya mtoto.


Rasilimali muhimu za kujifunza zaidi


Rejea za mada hii
  1. Cunningham FG, Leveno KJ, Bloom SL, Spong CY, Dashe JS, Hoffman BL, et al. Williams Obstetrics. 25th ed. New York: McGraw-Hill Education; 2018. p. 158–160.

  2. American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG). Prenatal development: How your baby grows during pregnancy [Internet]. ACOG; 2023 [cited 2025 Jun 17]. Available from: https://www.acog.org/womens-health/faqs/how-your-baby-grows-during-pregnancy

  3. Smith GCS, Pell JP, Cameron AD. Risk of perinatal death associated with reduced fetal movements in pregnancy. BMJ. 2003 Aug;327(7421):245–248.

  4. Royal College of Obstetricians and Gynaecologists (RCOG). Reduced fetal movements. Green-top Guideline No. 57. London: RCOG; 2011 [updated 2019; cited 2025 Jun 17]. Available from: https://www.rcog.org.uk/guidance/browse-all-guidance/green-top-guidelines/reduced-fetal-movements-gtg57/

  5. Norwitz ER, Schorge JO, Chaudhury P, et al. Obstetrics and Gynecology at a Glance. 4th ed. Wiley-Blackwell; 2013.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:07:24

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

bottom of page