top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Mangwella S, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Muda sahihi kusoma kipimo cha HIV SD bioline

Jibu kwa ufupi


Swali la mteja: "Nilipima kwa SD Bioline kikaonyesha mstari mmoja kwenye C. Baada ya saa tatu kikaonyesha mstari wa pili. Baadaye nikapima kwa Unigold kikasoma mstari mmoja, na zaidi ya mwaka imekuwa hivyo. Je, nina VVU?"


Jibu kwa ufupi: Hapana. Mstari uliotokea baada ya saa 3 si jibu halali. SD Bioline ilikuwa hasi ndani ya muda sahihi, na Unigold ni hasi – huna VVU kutokana na vipimo hivyo. Soma C ina maanisha nini.


Maelezo


Kipimo kinavyofanya kazi


  • Kina mistari mitatu: 1 (VVU-1), 2 (VVU-2) na C (udhibiti).

  • Damu na maji ya kipimo hutembea kupita mistari 1, 2 hadi C.

  • Mstari C huonyesha kipimo kimefanya kazi.

  • Kabla ya kuweka sampuli, mistari yote haipaswi kuonekana.


Kusoma majibu


  • Soma baada ya dakika 10, si zaidi ya dakika 20.

  • C pekee – hasi.

  • C pamoja na 1 au 2 – chanya; thibitisha.

  • Hakuna C – kipimo hakijafanya kazi; rudia.

  • Rangi nyekundu ikitawala dakika 10, subiri na soma kabla ya dakika 20.

  • Baada ya dakika 20 mstari hafifu unaweza kujitokeza kwa sababu ya kukauka – si jibu.


Mistari 1 na 2 pamoja


Ni nadra kuwa na VVU-1 na VVU-2 pamoja; mara nyingi ni kufanana kwa protini. Uthibitisho hufanyika maabara – soma Utofauti wa VVU-1 na VVU-2.


Utaratibu wa Tanzania


  • Kipimo cha kwanza – SD Bioline; kikiwa hasi, majibu ni hasi.

  • Kikiwa chanya – kipimo cha pili Unigold.

  • Vikitofautiana – kurudia au kipimo cha maabara kama ilivyoelekezwa; soma Majibu chanya ya VVU pasipo VVU.


Nini cha kufanya


  • Weka kengele dakika 10 na usome kabla ya dakika 20, kisha tupa kipimo mahali salama.

  • Usisome kipimo kilichowekwa pembeni kwa saa.

  • Kama hatari ilikuwa ndani ya wiki 12, rudia baada ya wiki 12.

  • Majibu yakitofautiana – nenda kituo cha afya.


Dalili za hatari


  • Wasiwasi mkubwa au mawazo ya kujidhuru baada ya majibu – ongea na mshauri nasaha mara moja.


Lini umwone daktari


  • Majibu chanya au yasiyoeleweka.

  • Vipimo viwili vinatofautiana.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Mstari wa pili umetokea baada ya saa 3, nina VVU?

Hapana. Majibu yanayosomwa baada ya dakika 20 si sahihi.

2. SD Bioline imesoma chanya na Unigold hasi, nifanyeje?

Hakuna hitimisho bado – rudia baada ya wiki 2 au kipimo cha maabara kama ulivyoelekezwa.

3. Mistari mitatu imetokea, nina VVU-1 na VVU-2?

Mara nyingi hapana – thibitisha maabara.

4. Kipimo kimesoma bila mstari C, ni hasi?

Hapana, kipimo hakijafanya kazi – tumia kingine.

5. Kaswende inaweza kufanya kipimo cha VVU kiwe chanya?

Mara chache baadhi ya magonjwa huleta chanya ya uongo – ndiyo maana kipimo cha pili hufanyika.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:17:51

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. World Health Organization. Consolidated guidelines on differentiated HIV testing services. Geneva: WHO; 2024.

  2. Ministry of Health Tanzania. National Guidelines for the Management of HIV and AIDS. 7th ed. Dodoma: NACP; 2019.

  3. Standard Diagnostics. SD BIOLINE HIV-1/2 3.0 – package insert.

bottom of page