Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Sospeter L, MD
2 Aprili 2026, 16:17:50

Majibu chanya ya VVU pasipo VVU
Majibu chanya ya kipimo cha HIV SD bioline licha ya kushuku maambukizi ya VVU, huweza kuwa chanya kwa mwenye kaswende, kichocho, minyoo, shambulio binafsi la kinga, ujauzito n.k. Majibu chanya yanapaswa kuthibitishwa kwa kipimo cha HIV Uni-Gold au vingine vyenye ufanisi zaidi.
Inawezekana kuwa na majibu chanya ya VVU wakati huna VVU?
Ndio unawezekana kuwa na majibu chanya( positive) kwa kipimo cha SD bioline wakati huna maambukizi hayo
Majibu chanya ya kipimo cha HIV SD bioline huweza kuwa chanya kwenye baadhi ya maambukizi ya virusi, bakteria, minyoo na baadhi ya hali kama ujauzito n.k
Magonjwa yanayoweza kuleta majibu chanya wakati huna VVU
Kuna magonjwa mbalimbali yanaweza kupelekea kupata majibu chanya ya VVU wakati huna VVU ambayo ni;
Maambukizi ya kirusi cha Epstein-Barr
Kiasi kibubwa cha bilirubin kwenye damu
Magonjwa shambulio bonafsi la mfumo wa kinga
Ugonjwa wa kaswende
Ugonjwa wa lupus
Ugonjwa wa lyme
Ugonjwa wa kichocho kutokana na kimelea schitosoma mansoni
Hali zinazoweza pelekea kupata majibu chanya wakati huna VVU
Hali zifuatazo zinaweza kupelekea kupata majibu chanya wakati huna maambukizi ya VVU;
Kuchanganya sampuli
Kusoma vibaya majibu ya kipimo ( mfano kusoma baada ya muda unaotakiwa)
Ujauzito
Kuchoma chanjo ya virusi mfano chanjo ya kirusi cha influenza
Kuchoma chanjo ya VVU
Kuamshwa kwa chembe B na CD5 za mfumo wa kinga ya mwili kuitikia maambukizi ya malaria
Vipimo vya kuthibitisha uwepo wa maambukizi wa VVU
Vipimo vya kuthibitisha uwepo wa maambukizi wa VVU ni
Kipimo cha HIV culture
Kipimo cha Western Blot (kilikuwa kinatumika sana zamani)
Neutralization Test
NAT
Kipimo cha HIV antijen Test
Je Kipimo cha HIV Uni-Gold hutosha kuthibitisha majibu chanya ya HIV
Kipimo cha Uni- Gold hupima antibodi zinazozalishwa na mwili dhibi ya kirusi, licha ya kuwa na ufanisi wa asilimia 98.8 kinaweza kutotoa majibu ya ukweli kwa baadhi ya nyakati hivyo vipimo vilivyoandikwa hapo juu ni vipimo vya kuthibitisha uhalari wa majibu chanya. Kwa sababu kwa nchi nyingi zinazoendelea hakuna uwezo wa kufanya vipimo hivyo kutokana na gharama, kipimo cha Uni-Gold hutosha kutoa majibu ya uthibitisho kwamba una mambukizi ya VVU baada ya kuwa na majibu chanya kwenye kipimo cha HIV SD bioline.
Ushauri kwako
Mara baada ya kujipima nyumbani au kupimwa hospitali na kujikuta kuwa na maambukizi ya VVU, unapswa kwenda hospitali kwa ajili ya uthibitisho wa majibu hayo kwa vipimo vingine muhimu kama HIV Uni-Gold au Culture pamoja na western blot.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:17:50
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
