top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Glory, MD

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Muundo na rangi ya haja kubwa kwa kichanga

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Njano, kijani, kahawia – kawaida. Nyeupe/kijivu, damu, nyeusi (baada ya siku 4) – hospitali leo. Soma Rangi ya kinyesi cha kawaida kwa mtoto.


Haja kubwa kwa mtoto mchanga
Haja kubwa kwa mtoto mchanga

Maelezo


Kwa umri


  • Siku 1–3 – meconium.

  • Siku 3–5 – kijani-kahawia.

  • Wiki 1+ (maziwa ya mama) – njano, mbegu, mara nyingi.

  • Wiki 1+ (kopo) – njano-kahawia, nzito, mara 1–4.

  • Wiki 4–6 – huweza kukaa siku kadhaa bila haja (maziwa ya mama).


Hatari


  • Nyeupe, kijivu, udongo – dharura.

  • Damu.

  • Nyeusi baada ya siku 4.

  • Majimaji mengi – soma Kuharisha.

  • Ngumu kama vijiwe, kulia sana.


Nini cha kufanya


  • Endelea kunyonyesha.

  • Andika mara ngapi na rangi wiki za mwanzo.

  • Piga picha ukiwa na shaka.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja mtoto akiwa na:


  • Haja nyeupe/kijivu.

  • Damu nyingi.

  • Kutopata haja saa 48 baada ya kuzaliwa.

  • Tumbo kuvimba na kutapika kijani.

  • Kulegea, macho kuingia ndani.


Lini umwone daktari



Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Kijani ni kawaida?

Ndiyo, mara nyingi.

2. Mara ngapi kwa siku?

Anayenyonya – 3–6 au zaidi; baadaye huweza kupungua.

3. Siku 3 bila haja (wiki 6)?

Kawaida kwa anayenyonya kama ni laini.

4. Haja nyeupe?

Dharura.

5. Mbegu kwenye haja?

Kawaida – mafuta ya maziwa.

6. Kopo ni tofauti?

Nzito zaidi, harufu kali.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:08:31

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Den Hertog J, et al. The defecation pattern of healthy term infants up to the age of 3 months. Arch Dis Child Fetal Neonatal Ed. 2012;97(6):F465–70.

  2. Hsiao CH, et al. Universal screening for biliary atresia using an infant stool color card in Taiwan. Hepatology. 2008;47(4):1233–40.

  3. World Health Organization. Pocket book of hospital care for children. 2nd ed. Geneva: WHO; 2013.

bottom of page