Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Mangwella S, MD
Dkt. Charles W, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Mwanamke aliehalibikiwa ujauzito anaweza kupata ujauzito mwingine ndani ya miezi 6?
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Unaweza kujaribu tena mara utakapojisikia tayari na damu imekoma. Anza folic acid sasa. Kama hutaki mimba sasa, anza uzazi wa mpango mara moja. Soma Mambo ya kufanya baada ya mimba kutoka.
Maelezo
Ushahidi
Uchambuzi wa tafiti (zaidi ya wanawake milioni 1) – mimba ndani ya miezi 6 ilikuwa na hatari ndogo zaidi ya kuharibika tena na ya kuzaa njiti.
Wanandoa walioanza kujaribu ndani ya miezi 3 walipata mimba haraka zaidi bila hatari ya ziada.
Wanaohitaji kusubiri au ushauri maalumu
Mimba zabibu (molar) – subiri hadi kipimo cha hCG kiwe sawa na ruhusa ya mtoa huduma.
Mimba nje ya kizazi iliyotibiwa kwa methotrexate – subiri miezi 3.
Mimba kuharibika mara 3 au zaidi, au baada ya miezi 3 ya ujauzito – uchunguzi kwanza; soma Mimba kuharibika miezi mitano.
Upungufu wa damu, maambukizi, au huzuni kubwa – tibu kwanza.
Nini cha kufanya
Subiri damu ikome na ujisikie tayari – soma Muda wa ngono baada ya mimba kutoka.
Folic acid kila siku kabla ya kushika mimba.
Kula vizuri; madini chuma kama ulipoteza damu nyingi.
Pima kisukari, presha, VVU na kaswende kama hujapima.
Anza kliniki mapema mimba ikiingia – ultrasound ya mapema.
Soma Kikokotoo: uwezekano wa kushika mimba baada ya mimba kutoka.
Dalili za hatari
Nenda kituo cha afya mara moja ukiwa na:
Damu nyingi, homa au uchafu wenye harufu baada ya mimba kutoka.
Mimba mpya yenye maumivu makali upande mmoja au damu – soma Dalili za mimba kuharibika.
Lini umwone daktari
Mimba imeharibika mara 2 au zaidi.
Hujashika mimba baada ya mwaka 1 wa kujaribu (miezi 6 kama una miaka 35+).
Huzuni au wasiwasi mkubwa baada ya kupoteza mimba.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Naweza kushika mimba mwezi mmoja baada ya mimba kutoka?
Ndiyo, yai linaweza kutoka mapema.
2. Ni lazima kusubiri miezi 6?
Si lazima kwa mimba ya mapema; jambo kuu ni kuwa tayari.
3. Mimba ya haraka itaharibika tena?
Tafiti hazionyeshi hatari kubwa zaidi.
4. Nisubiri hedhi ya kwanza?
Si lazima, lakini husaidia kukadiria umri wa mimba mpya.
5. Baada ya mimba zabibu nisubiri muda gani?
Hadi hCG iwe sawa na mtoa huduma aruhusu.
6. Folic acid nianze lini?
Sasa, kabla ya kushika mimba.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:15
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Kangatharan C, Labram S, Bhattacharya S. Interpregnancy interval following miscarriage and adverse pregnancy outcomes: systematic review and meta-analysis. Hum Reprod Update. 2017;23(2):221–31.
Schliep KC, et al. Trying to conceive after an early pregnancy loss: an assessment on how long couples should wait. Obstet Gynecol. 2016;127(2):204–12.
World Health Organization. Report of a WHO technical consultation on birth spacing. Geneva: WHO; 2007.

