Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Mzunguko wa hedhi ukoje?
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Hesabu kuanzia siku ya kwanza ya damu. Siku za hatari ni siku 5 kabla ya uovuleshaji na siku yenyewe – kwa mzunguko wa 28, karibu siku ya 9 hadi 14 (si 12 hadi 17). Soma Mzunguko wa hedhi.
Maelezo
Mzunguko wa kawaida
Urefu – siku 24 hadi 38 kwa watu wazima; 21 hadi 45 miaka 2 ya mwanzo baada ya hedhi ya kwanza.
Siku za damu – hadi 8 (mara nyingi 3 hadi 7).
Kiasi cha damu – mara nyingi mililita 30 hadi 40; zaidi ya 80 ni nyingi.
Tofauti kati ya mizunguko – hadi siku 7 hadi 9 ni kawaida.
Hedhi ya kwanza – wastani wa miaka 12, baada ya matiti kuota na nywele za sehemu za siri.
Siku za hatari
Uovuleshaji ≈ siku 14 kabla ya hedhi inayofuata.
Dirisha la rutuba – siku 5 kabla ya uovuleshaji + siku ya uovuleshaji (siku 6).
Mzunguko wa 28 – uovuleshaji ≈ siku ya 14; rutuba ≈ siku 9 hadi 14 – soma Mzunguko wa siku 28.
Mzunguko wa 35 – uovuleshaji ≈ siku ya 21; rutuba ≈ siku 16 hadi 21.
Idadi ya siku za damu haibadilishi hesabu hii.
Nini cha kufanya
Andika siku ya kwanza ya kila hedhi kwa miezi 3 hadi 6 kujua mzunguko wako.
Ute kama yai bichi huashiria siku za rutuba.
Kama hutaki mimba, tumia njia ya kisasa – kalenda peke yake si ya uhakika.
Dalili za hatari
Damu nyingi sana – pedi kubwa kujaa kila saa, kizunguzungu – kituo cha afya.
Hedhi imechelewa na maumivu makali upande mmoja.
Lini umwone daktari
Mzunguko mfupi kuliko siku 21 au mrefu kuliko 45.
Hedhi zaidi ya siku 8.
Damu kati ya hedhi au baada ya tendo.
Hakuna hedhi kufikia miaka 15.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Mzunguko wangu ni siku 28, siku za hatari ni zipi?
Karibu siku ya 9 hadi 14 tangu siku ya kwanza ya hedhi.
2. Nahesabuje mzunguko?
Kuanzia siku ya kwanza ya damu hadi siku ya kwanza ya hedhi inayofuata.
3. Hedhi ya siku 2 ni kawaida?
Inaweza kuwa kawaida kama ni ya mpangilio.
4. Mzunguko kubadilika kila mwezi ni tatizo?
Tofauti ya siku chache ni kawaida; zaidi ya siku 9 mwone mtoa huduma.
5. Binti wa miaka 13 mzunguko wake hauna mpangilio, ni kawaida?
Ndiyo, miaka 2 ya mwanzo ni kawaida.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:21
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Munro MG, Critchley HOD, Fraser IS. The two FIGO systems for normal and abnormal uterine bleeding symptoms: 2018 revisions. Int J Gynaecol Obstet. 2018;143(3):393–408.
American College of Obstetricians and Gynecologists. Menstruation in girls and adolescents: using the menstrual cycle as a vital sign. Committee Opinion No. 651. 2015.
Wilcox AJ, Dunson D, Baird DD. The timing of the 'fertile window' in the menstrual cycle. BMJ. 2000;321:1259–62.

