top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Mangwella S, MD

Dkt. Benjamin L, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Nina mimba ya mwezi mmoja na nusu naweza tumia amlodipine kushusha presha?

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Kama umemeza amlodipine bila kujua una mimba, usihofu sana – hatari inaonekana ndogo. Lakini mwone daktari sasa ili akubadilishie dawa inayopendekezwa ujauzitoni. Presha isiyodhibitiwa ni hatari zaidi kuliko kubadilisha dawa.


Maelezo


Ushahidi kuhusu amlodipine


  • Ripoti za mwanzo zilikuwa za wanawake wachache tu.

  • Tafiti mpya za binadamu (k.m. Mito 2019) hazijaonyesha ongezeko kubwa la kasoro za kuzaliwa kwa waliotumia miezi 3 ya kwanza.

  • Baadhi ya tafiti zimehusisha dawa za presha kwa ujumla na mtoto kukua kidogo – presha yenyewe pia huchangia.


Dawa zinazopendekezwa ujauzitoni



Nini cha kufanya


  • Usiache dawa ghafla.

  • Nenda kliniki ya ujauzito mapema – soma Mahudhurio ya kliniki.

  • Pima presha mara kwa mara.

  • Punguza chumvi, fanya mazoezi mepesi, epuka pombe na sigara.

  • Kama una presha na unapanga mimba – ongea na daktari kubadilisha dawa kabla.


Dalili za hatari


Nenda hospitali mara moja ukiwa na:


  • Kichwa kuuma sana, macho kuona ukungu au nyota.

  • Maumivu chini ya mbavu upande wa kulia.

  • Uso, mikono kuvimba ghafla.

  • Degedege.

  • Presha 160/110 au zaidi.


Lini umwone daktari



Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Nimetumia amlodipine nikiwa na mimba bila kujua, mtoto ataathirika?

Tafiti za karibuni zinaonyesha hatari ndogo; mwone daktari kubadilisha dawa na kufuatilia mimba.

2. Niache amlodipine mara moja?

Hapana, badilisha kwa ushauri wa daktari ili presha isipande.

3. Dawa gani ya presha salama kwa mjamzito?

Methyldopa, nifedipine au labetalol kwa ushauri.

4. Presha kwa mjamzito ni hatari?

Ndiyo, huweza kuleta kifafa cha mimba na matatizo kwa mtoto.

5. Enalapril inafaa ujauzitoni?

Hapana, inaweza kuathiri figo na fuvu la mtoto.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:15

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

  2. Mito A, et al. Safety of amlodipine in early pregnancy. J Am Heart Assoc. 2019;8(15):e012093.

  3. World Health Organization. WHO recommendations on drug treatment for non-severe hypertension in pregnancy. Geneva: WHO; 2020.

  4. Ahn HK, et al. Exposure to amlodipine in the first trimester of pregnancy and during breastfeeding. Hypertens Pregnancy. 2007;26(2):179–87.

bottom of page