Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Mangwella S, M.D
Dkt. AdolfS, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Nini kinafuata baada ya kuanza PEP?
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Maliza dawa siku 28, hudhuria vipimo vya wiki 6 na wiki 12, na tumia kondomu hadi utakapothibitishwa huna VVU. Kipimo cha wiki 12 kikiwa hasi, hujaambukizwa kutokana na tukio hilo.
Maelezo
Kabla ya kuanza
Kipimo cha VVU – kama ni chanya, unaanza matibabu ya VVU badala ya PEP.
Kama vinapatikana: kipimo cha figo, ini, damu, homa ya ini B na mimba.
Kama inawezekana, hali ya VVU ya mtu aliyesababisha hatari.
Wakati wa PEP
Dawa kila siku kwa siku 28, saa ile ile.
Ufuatiliaji wa maudhi – mara nyingi wiki ya 2; soma Je, kuna madhara ya kutumia PEP muda mrefu?.
Kama maudhi hayavumiliki, dawa hubadilishwa – usiache mwenyewe.
Baada ya PEP
Kipimo cha VVU wiki 6 na wiki 12.
Kama hatari ilikuwa ya ngono – pia vipimo vya kaswende na magonjwa mengine ya zinaa.
Kama hatari bado ipo – uliza kuhusu PrEP.
Nini cha kufanya
Usikose dozi – weka kengele ya simu.
Tumia kondomu na usichangie damu hadi kipimo cha wiki 12 kiwe hasi.
Mama anayenyonyesha aongee na mtoa huduma kuhusu kunyonyesha katika kipindi hiki.
Beba kadi ya PEP kila unapoenda kituo cha afya.
Dalili za hatari
Nenda kituo cha afya mara moja ukiwa na:
Homa, vipele, koo kuuma, mitoki kuvimba, uchovu mkubwa – huenda ni maambukizi mapya ya VVU; utapimwa na kupelekwa CTC kama ni chanya.
Vipele vikali au macho kuwa ya njano.
Kutapika kila dozi.
Lini umwone daktari
Umekosa dozi zaidi ya 2.
Umepata hatari nyingine ya VVU ukiwa kwenye PEP.
Una wasiwasi mkubwa – soma VVU na UKIMWI.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Nimeanza PEP, nitapimwa tena lini?
Wiki 6 na wiki 12 baada ya tukio la hatari.
2. Nimepimwa wiki 6 hasi, nimepona?
Ni habari njema, lakini subiri kipimo cha wiki 12 kuthibitisha.
3. PEP inatumika kwa siku ngapi?
Siku 28 mfululizo.
4. Nimepata homa nikiwa kwenye PEP, ni VVU?
Inaweza kuwa maudhi au ugonjwa mwingine, lakini nenda ukapimwe mara moja.
5. Naweza kufanya ngono nikiwa kwenye PEP?
Tumia kondomu kila mara hadi kipimo cha wiki 12 kiwe hasi.
6. Nimesahau dozi moja ya PEP, nifanyeje?
Meza mara moja ukikumbuka, kisha endelea kama kawaida.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.
Ministry of Health Tanzania. National Guidelines for the Management of HIV and AIDS. 7th ed. Dodoma: NACP; 2019.
World Health Organization. Guidelines for HIV post-exposure prophylaxis. Geneva: WHO; 2024.

