top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt Salome A, MD

Dkt. Mangwella S, M.D

31 Oktoba 2026, 15:23:37

PEP na pombe

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Ni bora kuepuka au kupunguza pombe kwa siku 28 za PEP. Jambo muhimu zaidi ni kutokosa dozi hata moja. Soma Nini kinafuata baada ya kuanza PEP.


Maelezo


Kwa nini usinywe pombe


  • Kusahau dozi – PEP inahitaji dozi kila siku saa ile ile.

  • Maudhi kuzidi – kichefuchefu, kichwa kuuma, uchovu.

  • Ini – unywaji mwingi huongeza mzigo kwa ini.

  • Maamuzi – pombe huongeza hatari ya ngono bila kinga tena.


Nini cha kufanya


  • Weka kengele ya simu ya dozi.

  • Kama utakunywa, kunywa kidogo na usikose dozi.

  • Kunywa maji ya kutosha.

  • Tumia kondomu hadi upimwe wiki 12.

  • Soma Madhara ya PEP muda mrefu.


Dalili za hatari


  • Kutapika kila dozi, macho kuwa ya njano, vipele vikali – kituo cha afya mara moja.


Lini umwone daktari


  • Umesahau dozi zaidi ya 2.

  • Unakunywa pombe kila siku na unahitaji msaada wa kupunguza.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Naweza kunywa bia nikitumia PEP?

Kidogo hakizuii dawa, lakini ni bora kuepuka.

2. Pombe inapunguza nguvu ya PEP?

Hakuna ushahidi wa moja kwa moja; hatari kubwa ni kusahau dozi.

3. Nimekunywa pombe nikasahau dozi, nifanyeje?

Meza mara moja ukikumbuka, kisha endelea kama kawaida.

4. Pombe na PEP vinaweza kuharibu ini?

Unywaji mwingi huongeza mzigo kwa ini – epuka.

5. Baada ya kumaliza PEP naweza kunywa?

Ndiyo, kwa kiasi.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:17

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Aidsmap. Alcohol and HIV. NAM; 2023.

  2. World Health Organization. Guidelines for HIV post-exposure prophylaxis. Geneva: WHO; 2024.

bottom of page