top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Mangwella S, MD

Dkt. Lugonda B, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Tinidazole inatibu gono?

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Tinidazole haitibu gono. Ukitumia peke yake kwa gono, hutapona na unaweza kuendelea kuambukiza. Soma Kisonono na Matibabu ya gono.


Maelezo


Tinidazole hutibu


  • Trikomona (ugonjwa wa zinaa).

  • Amiba.

  • Giardia.

  • Bakteria vaginosis.


Kwa nini watu huchanganya


  • Usaha au uchafu sehemu za siri hudhaniwa kuwa gono kila mara.

  • Matibabu ya dalili hulenga vimelea kadhaa – ndiyo maana tinidazole au metronidazole hutolewa pamoja na dawa nyingine.

  • Soma Metronidazole inatibu nini.


Tahadhari ya tinidazole


  • Usinywe pombe wakati wa dawa na siku 3 baada – huleta kutapika na moyo kwenda mbio.

  • Ladha ya chuma mdomoni, kichefuchefu.

  • Mjamzito wa miezi 3 ya kwanza – ushauri wa daktari.


Nini cha kufanya


  • Pima kituo cha afya kabla ya kununua dawa.

  • Maliza dawa zote ulizopewa.

  • Mwenzi atibiwe pia; epuka ngono hadi wote mmalize matibabu.

  • Pima VVU na kaswende.

  • Usinunue dawa bila ushauri – huleta usugu wa vimelea.


Dalili za hatari


  • Korodani kuvimba na kuuma, maumivu ya tumbo la chini na homa – kituo cha afya mara moja.


Lini umwone daktari


  • Dalili hazijaisha baada ya matibabu.

  • Dalili zinajirudia.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Nimetumia tinidazole na usaha bado unatoka, kwa nini?

Tinidazole haitibu gono – nenda kituo cha afya upate dawa sahihi.

2. Tinidazole na metronidazole ni sawa?

Ni jamii moja na hutibu magonjwa yanayofanana.

3. Naweza kunywa pombe nikitumia tinidazole?

Hapana, subiri siku 3 baada ya dozi ya mwisho.

4. Gono hutibiwa kwa dawa gani?

Antibiotiki maalumu kwa ushauri wa mtoa huduma kulingana na mwongozo wa Taifa.

5. Mwenzi wangu atibiwe pia?

Ndiyo, vinginevyo utaambukizwa tena.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:13

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

  2. Workowski KA, et al. Sexually Transmitted Infections Treatment Guidelines, 2021. MMWR Recomm Rep. 2021;70(4):1–187.

  3. Fung HB, Doan TL. Tinidazole: a nitroimidazole antiprotozoal agent. Clin Ther. 2005;27(12):1859–84.

bottom of page