top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Glory, MD

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Uchafu mweupe ukeni wakati wa ujauzito

Jibu kwa ufupi


Swali la mteja: "Daktari, mimi ni mjamzito na natokwa na uchafu mweupe kama maziwa mgando. Ni kawaida au kuna tatizo?"


Jibu kwa ufupi: Kama una muwasho au kuungua, mara nyingi ni fangasi – mwambie mtoa huduma upate dawa ya kuweka ukeni. Usimeze dawa za fangasi bila ushauri. Soma Fangasi ukeni.



Maelezo


Kawaida



Si kawaida


  • Mzito kama maziwa mgando, muwasho – fangasi.

  • Kijivu, harufu ya samaki – bakteria vaginosis; soma BV kwa mjamzito.

  • Njano-kijani, povu, harufu – trikomona.

  • Maji mengi mepesi yanayotiririka – chupa ya uzazi huenda imepasuka (dharura).

  • Damu au ute wenye damu – mwone mtoa huduma.


Nini cha kufanya


  • Fangasi – dawa ya kuweka ukeni (mf. clotrimazole) kwa siku 7 kwa maelekezo.

  • Usiweke vitu wala dawa za kienyeji ukeni; usisafishe ndani.

  • Chupi za pamba; kausha vizuri.

  • Pima sukari ya ujauzito kama fangasi hujirudia.

  • Soma Dawa za uchafu mweupe ukeni na Uteute mweupe kwa mjamzito.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja ukiwa na:


  • Maji mengi kutoka ukeni.

  • Damu ukeni.

  • Homa na maumivu ya tumbo.

  • Mtoto kupunguza kucheza.


Lini umwone daktari


  • Uchafu wenye muwasho, harufu au rangi isiyo ya kawaida.

  • Kuungua ukikojoa.

  • Fangasi zinazorudi.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Uchafu mweupe ujauzitoni ni kawaida?

Mwepesi bila harufu ndiyo.

2. Uchafu kama maziwa mgando ni nini?

Mara nyingi fangasi.

3. Fangasi ujauzitoni zinamdhuru mtoto?

Kwa kawaida hapana; zitibiwe kwa faraja.

4. Nimeze fluconazole?

Hapana ujauzitoni; dawa ya kuweka ukeni hupendelewa.

5. Uchafu wenye harufu ni hatari?

Unaweza kuchangia kuzaa njiti; pima.

6. Maji mepesi mengi ni nini?

Huenda chupa imepasuka – hospitali.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:07:37

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Workowski KA, et al. Sexually Transmitted Infections Treatment Guidelines, 2021 – Vulvovaginal candidiasis in pregnancy. MMWR Recomm Rep. 2021;70(4).

  2. Mølgaard-Nielsen D, et al. Association between use of oral fluconazole during pregnancy and risk of spontaneous abortion and stillbirth. JAMA. 2016;315(1):58–67.

  3. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

bottom of page