Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Benjamin L, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Unasisimuaje G spoti?
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Mguso wa taratibu kwenye ukuta wa mbele wa uke, pamoja na kisimi, kwa ridhaa na mawasiliano. Soma G spoti inapatikana wapi?.

Maelezo
Kinachoweza kusaidia
Maandalizi ya muda mrefu – msisimko huongeza unyeti wa eneo hili.
Kidole safi, kucha fupi, kilainishi.
Mwendo wa taratibu wa "njoo" kuelekea ukuta wa mbele.
Mapozi – mwanamke juu au mwanamke kulala tumbo – soma Pozi la mwanamke kufika kileleni.
Kugusa kisimi kwa wakati mmoja huongeza raha kwa wengi.
Mambo ya kujua
Hisia ya kutaka kukojoa mwanzoni ni kawaida – kojoa kabla ya tendo.
Majimaji yanayotoka kwa baadhi wakati wa kilele – soma Maji ya mwanamke aliyekojozwa.
Wanawake wengine hawahisi tofauti – ni kawaida, si tatizo.
Nini cha kufanya
Ridhaa ya wote wawili; acha mwenzi akiomba.
Usafi wa mikono na vifaa; kondomu kwenye vifaa vya kuchezea vikishirikiwa.
Usitumie nguvu – huchubua uke.
Kojoa baada ya tendo kupunguza UTI.
Dalili za hatari
Maumivu makali au damu nyingi baada ya tendo – mwone mtoa huduma.
Lini umwone daktari
Maumivu wakati wa tendo yanajirudia.
Kuungua ukikojoa baada ya tendo.
Kutofika kileleni kunakusumbua.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. G spoti inasisimuliwaje?
Kwa mguso wa taratibu kwenye ukuta wa mbele wa uke.
2. Kila mwanamke anahisi raha G spoti ikiguswa?
Hapana, hutofautiana.
3. Kuhisi kukojoa ni kawaida?
Ndiyo, kwa sababu iko karibu na mrija wa mkojo.
4. Kilainishi kinahitajika?
Kinasaidia kupunguza msuguano.
5. Kisimi ni muhimu zaidi?
Kwa wanawake wengi, ndiyo.
6. Ridhaa ni muhimu?
Ndiyo, kila wakati.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:17
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Vieira-Baptista P, et al. G-spot: fact or fiction? A systematic review. Sex Med. 2021;9(5):100435.
Kilchevsky A, et al. Is the female G-spot truly a distinct anatomic entity? J Sex Med. 2012;9(3):719–26.

