top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:43

Uume wangu unatoa usahaa lakini sina maumivu yoyote hii nitatizo gani?

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Usaha uumeni = nenda kituo cha afya hata bila maumivu. Wewe na mwenzi mtibiwe pamoja; acheni ngono hadi siku 7 baada ya tiba. Soma Uume kutoa usaha.


Maelezo


Visababishi


  • Klamidia – ute mweupe au mwepesi, mara nyingi bila maumivu.

  • Gono – usaha mzito wa njano-kijani; maumivu huweza kuwa kidogo mwanzoni.

  • Mycoplasma genitalium na trikomonasi – ute unaojirudia baada ya tiba.

  • Visababishi visivyo vya zinaa – maambukizi ya tezi dume au mkojo (si mara nyingi kwa vijana).


Kwa nini usisubiri


  • Kuvimba korodani (epididimaitisi) na kupungua uwezo wa kuzaa.

  • Kumwambukiza mwenzi – PID, mimba nje ya kizazi, ugumba.

  • Huongeza uwezekano wa kupata au kuambukiza VVU.

  • Soma Madhara ya kutotibu usaha sehemu za siri.


Nini cha kufanya


  • Usinunue antibayotiki mwenyewe – gono imekuwa sugu kwa dawa nyingi.

  • Pima VVU na kaswende pia.

  • Mwenzi (au wenzi wa miezi 2 iliyopita) apimwe na atibiwe.

  • Tumia kondomu kila mara.

  • Soma Vimelea vya usaha na Matibabu kamili ya gono.


Dalili za hatari


Kituo cha afya haraka ukiwa na:


  • Korodani kuvimba au kuuma.

  • Homa, maumivu ya viungo au vipele mwilini.

  • Kushindwa kukojoa.


Lini umwone daktari



Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Sina maumivu, ni lazima niende hospitali?

Ndiyo; usaha ni dalili ya maambukizi.

2. Ni ugonjwa gani mara nyingi?

Klamidia au gono.

3. Mpenzi wangu atibiwe?

Ndiyo, hata kama hana dalili.

4. Naweza kununua dawa duka la dawa?

Hapana; tiba ya STG inahitaji mtoa huduma.

5. Nikae bila ngono muda gani?

Hadi siku 7 baada ya tiba yako na ya mwenzi.

6. Usaha umerudi baada ya dawa, kwa nini?

Maambukizi mapya, mwenzi hakutibiwa, au vimelea sugu – rudi kituoni.

7. Unaweza kuathiri uwezo wa kuzaa?

Ndiyo, usipotibiwa.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:07:37

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. World Health Organization. Guidelines for the management of symptomatic sexually transmitted infections. Geneva: WHO; 2021.

  2. Workowski KA, et al. Sexually Transmitted Infections Treatment Guidelines, 2021. MMWR Recomm Rep. 2021;70(4):1–187.

  3. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

bottom of page