top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Sospeter B, MD

13 Desemba 2020 13:47:01

Uume kutoa usaha
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Uume kutoa usaha

Uume kutoa usaha ni dalili mojawapo ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa katika mrija wa urethra, tatizo hili huwapata wanaume wengi walio kwenye kipindi cha kufanya ngono na haswa vijana wadogo. Kwa maelezo zaidi unashauriwa kusoma zaidi makala inayohusu magonjwa ya zinaa haswa ugonjwa wa kisonono na gonorrhea (gono).


Dalili


Dalili ya kutoa usaha kwenye uume huweza kumaanisha ugonjwa wa zinaa endapo itaambatana na dalili zifuatazo;


  • Usaha kutoka wenyewe

  • Uume kutoa usaha wakati wa kukojoa

  • Maumivu ya uume wakati wa kukojoa

  • Muwasho ndani ya uume wakati wa kukojoa


Kisababishi


Kisababishi cha kutoka usaha kwenye tundu la uume ni maambukizi kwenye mrija wa urethra na hufahamika kitiba kama 'urethritis'


Ni vimelea gani vya maradhi husababisha kutokwa na usaha kwenye uume?


Vimelea wanaofahamika kusababisha uume kutoa usaha ni;


  • Chlamydia trachomatis

  • Neisseria gonorrhoeae


Kuna vimelea na viini wengine wanaosababisha uume kutoa usaha?


Ndio kuna viini na vimelea vingine vya maradhi vinavyoweza pelekea uume kutoa usaha ambavyo ni;


  • Mycoplasma genitalium

  • Trichomonas vaginalis

  • Kirusi herpes simplex

  • Kirusi adenovirus


Uume kutoa usaha huwapata kina nani?


Kutoka na usaha sehemu za siri hutokea kwa vijawa wa umri wowote ule, hii ni kwa sababu kipindi hiki vijana hushiriki sana ngono na wakati mwingine, kuwa na wapenzi wengi na bila kutumia kinga.


Vipimo


Mara nyingi vipimo havihitahijiki kufanyika ili kutambua tatizo, dalili tu inatosha kusema ni ugonjwa gani mtu anaugua, endapo vitahitajika, vipimo vifuatavyo vinaweza kufanyika;


  • Kipimo cha mkojo(urine analysis)- kinatakiwa kuonyesha angalau idadi ya chembe nyeupe za damu zinazofika 10

  • Kipimo chanya cha leukocyte esterase

  • Kipimo cha kuotesha vimelea na kutambua dawa gani inatibu (culture na sensitivity) kwa wagonjwa ambao wameshatumia dawa na bado hawajapona


Matibabu


Ili kuweza kufahamu kuhusu matibabu ya kutokwa na usaha sehemu za siri ingia kwenye makala zinazozungumzi kuhusu 'usaha sehemu za siri', 'dawa za gono', 'dawa za kisonono' na maambukizi ya magonjwa ya zinaa.


Kumbuka tatizo la kutokwa na usaha sehemu za siri huwa halitibiwi na dawa moja. Unashauriwa kuwasiliana na daktari wako ili kupata maelekezo zaidi ya matumizi sahihi na namna ya kutumia dawa ili kuepuka usugu wa dawa kwenye viini hivi vya maradhi.


Kinga ya uume kutoa usaha


Njia pekee ya kujikinga na uume kutoa usaha ni kuzuia maambukizi ya magonjwa haya kwa kuacha kufanya ngono, endapo utashindwa basi fanya mambo yafuatayo;


  • Tumia kondomu kisahihi kila unaposhiriki ngono

  • Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu ambaye hana maambukizi

  • Soma zaidi kuhusu makala za magonjwa ya zinaa ili kufahamu namna ya kujikinga

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 19:54:12

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.Urethral Discharge. https://accessmedicine.mhmedical.com/content.aspx?bookid=369&sectionid=39914779#. Imechukuliwa 11.12.2020
2.UDS.https://www.ulyclinic.com/urethral-discharge-syndrome-uds. Imechukuliwa 11.12.2020
3. American family of physician. Diagnosis and Treatment of Urethritis in Men. https://www.aafp.org/afp/2010/0401/p873.html. Imechukuliwa 11.12.2020

bottom of page