top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Lugonda B, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Uwezekano wa Kupata Mimba Baada ya Kujifungua

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Asiyenyonyesha – anza uzazi wa mpango kabla ya siku 21. Anayenyonyesha pekee – LAM hulinda hadi miezi 6 kama masharti yote yapo. Soma Uzazi wa mpango baada ya kujifungua.


Maelezo


Yai hurudi lini


  • Hunyonyeshi kabisa – mapema siku 25; wengi wiki 6–8; hedhi wiki 6–12.

  • Unakamua au kunyonyesha kwa sehemu – mapema kuliko anayenyonyesha pekee.

  • Unanyonyesha pekee – mara nyingi baada ya miezi 6 au zaidi, lakini huweza mapema.


Masharti ya LAM


  • Mtoto chini ya miezi 6.

  • Hedhi haijarudi.

  • Kunyonyesha pekee, mchana na usiku, bila mapengo ya zaidi ya saa 4–6.

  • Sharti moja likikosekana – njia nyingine; soma Kunyonyesha kama uzazi wa mpango.


Nini cha kufanya


  • Anza uzazi wa mpango mapema – vidonge vya projestini pekee, kipandikizi, kitanzi; soma Vidonge salama.

  • Subirini angalau miezi 18–24 kabla ya mimba nyingine kwa afya ya mama na mtoto.

  • Soma Ngono baada ya kujifungua.


Dalili za hatari


  • Maumivu makali upande mmoja na dalili za ujauzito – hospitali mara moja.


Lini umwone daktari


  • Dalili za ujauzito bila hedhi kurudi – pima mimba.

  • Unataka kuanza uzazi wa mpango.

  • Hedhi haijarudi miezi 6 baada ya kuacha kunyonyesha.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Naweza kupata mimba kabla ya hedhi kurudi?

Ndiyo.

2. Sinyonyeshi, yai hurudi lini?

Mapema kama siku 25.

3. Kunyonyesha kunazuia mimba?

Kunyonyesha pekee kwa masharti ya LAM ndiyo, hadi miezi 6.

4. Nakamua maziwa, niko salama?

Hapana kabisa; tumia njia nyingine.

5. Nisubiri muda gani kabla ya mimba nyingine?

Angalau miezi 18–24.

6. Njia ipi inafaa kwa anayenyonyesha?

Projestini pekee, kipandikizi, kitanzi au LAM.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:21

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Jackson E, Glasier A. Return of ovulation and menses in postpartum nonlactating women: a systematic review. Obstet Gynecol. 2011;117(3):657–62.

  2. World Health Organization. Family planning: a global handbook for providers. 2022 ed. Geneva: WHO; 2022.

  3. World Health Organization. Report of a WHO technical consultation on birth spacing. Geneva: WHO; 2007.

  4. Van der Wijden C, Manion C. Lactational amenorrhoea method for family planning. Cochrane Database Syst Rev. 2015;(10):CD001329.

bottom of page