top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Sospeter B, MD

Dkt. Charles W, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:43

Vidonge vya majira wakati wa kunyonyesha

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Ukinyonyesha, tumia vidonge vya projestini pekee au njia nyingine zisizo na estrojeni. Vichocheo viwili baada ya miezi 6. Soma Kunyonyesha kama njia ya uzazi wa mpango.


Maelezo


Ratiba kwa mama anayenyonyesha (WHO)


  • Chini ya wiki 6 – usitumie vichocheo viwili.

  • Wiki 6 hadi miezi 6, ukinyonyesha zaidi – kwa kawaida epuka vichocheo viwili.

  • Miezi 6 na zaidi – vichocheo viwili vinaweza kutumika.

  • Vidonge vya projestini pekee – vinaweza kuanzwa mapema baada ya kujifungua.


Njia nyingine zinazofaa


  • Kipandikizi.

  • Sindano ya Depo.

  • Kitanzi – ndani ya saa 48 au baada ya wiki 4.

  • Kunyonyesha pekee (LAM) – hadi miezi 6 kama hedhi haijarudi na mtoto ananyonya maziwa ya mama tu.


Nini cha kufanya



Dalili za hatari


  • Mguu mmoja kuvimba na kuuma, kupumua kwa shida, maumivu ya kifua baada ya kujifungua – hospitali mara moja.


Lini umwone daktari


  • Maziwa yamepungua baada ya kuanza vidonge.

  • Hedhi imerudi ukiwa kwenye LAM.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Naweza kutumia vidonge vya majira nikinyonyesha?

Ndiyo, vya projestini pekee.

2. Vidonge vya vichocheo viwili vinapunguza maziwa?

Vinaweza, hasa miezi ya mwanzo.

3. Nianze vidonge lini baada ya kujifungua?

Vya projestini mapema; vya vichocheo viwili baada ya miezi 6 ukinyonyesha zaidi.

4. Vidonge vinamdhuru mtoto?

Vya projestini havina madhara kwa mtoto.

5. Kunyonyesha pekee kunazuia mimba?

Ndiyo, hadi miezi 6 ukitimiza masharti yote.

6. Nikichelewa kumeza kidonge cha projestini?

Tumia kondomu siku 2.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:21

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. World Health Organization. Medical eligibility criteria for contraceptive use. 5th ed. Geneva: WHO; 2015.

  2. WHO, Johns Hopkins CCP. Family planning: a global handbook for providers. 2022 update. Baltimore and Geneva; 2022.

bottom of page