top of page

Maelezo ya majibu ya maswali mbalimbali ya kiafya

Chakula cha mgonjwa wa seli mundu

Seli mundu ni ugonjwa unaotokana na udhaifu katika umbo la chembe nyekundu ya damu, ugonjwa huu hurithiwa kutoka kwa baba na mama wenye vinasaba vya ugonjwa huu.

Kuishi maisha bora na ualbino

Tatizo la u albino huambatana na madhaifu kwenye ngozi na macho. Mtu mwenye u albino anaweza kupata matibabu ya mazingira kwa ajiri ya kupunguza au kuepuka madhara yanayoweza kutokea. kama yaliyoorodheshwa hapa chini.

Njia zisizoeneza Virusi vya UKIMWI

Kushikana mikono, kukumbatiana, kubusiana kwa midomo iliyofungwa, kula au kunywa pamoja, kutumia vyombo pamoja, kutumia choo, bafu au kuogelea pamoja, kulala kitanda kimoja, kukohoa au kupiga chafya karibu na mtu mwenye VVU, kuumwa na mbu au wadudu wengine, na kugusana kwa ngozi isiyokuwa na jeraha. Njia hizi hazitoi mazingira yanayofaa kwa virusi vya UKIMWI kuingia mwilini. Kuelewa njia hizi husaidia kuondoa hofu na unyanyapaa.

Njia zinazoeneza virusi vya UKIMWI

VVU huenea hasa kupitia ngono bila kinga, kujichoma sindano yenye majimaji ya damu ya mtu mwenye VVU, na kutoka kwa mama mwenye VVU kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito, kujifungua au kunyonyesha. Kujua njia hizi za maambukizi husaidia kutambua hatari halisi na kuchukua hatua madhubuti za kujikinga na VVU.

Bidhaa za hedhi za kupachika ukeni

Bidhaa kama tamponi, vikombe na diski za hedhi, hutofautiana katika namna zinavyokusanya au kunyonya damu, muda wa matumizi na mahitaji ya usafi, hivyo si bidhaa zinazotumika kwa utaratibu mmoja. Kujua tofauti hizi, namna ya kuzitumia na kuzisafisha, pamoja na kutambua dalili zinazohitaji kuacha matumizi na kutafuta ushauri wa kitabibu, husaidia mwanamke kuchagua bidhaa inayomfaa kwa usalama.

Taulo za kike (pedi)

Haikusudii tu kunyonya damu ya hedhi; aina ya pedi unayochagua, muda unaoitumia na jinsi unavyotunza usafi vinaweza kuathiri afya ya ngozi na sehemu za siri. Kuelewa jinsi unyevunyevu, msuguano, manukato na muda wa matumizi vinavyoweza kuathiri ngozi, pamoja na kutambua tofauti kati ya muwasho unaoweza kusababishwa na pedi na dalili za maambukizi, ni muhimu kwa matumizi salama na yenye afya ya pedi.

bottom of page