Mwandishi:
Mhariri:
ULY clinic
Dkt. Peter A, MD
18 Aprili 2020, 08:30:45

Dalili za matumizi ya dawa za kulevya
Madawa ya kulevya ni aina mbalimbali za dawa ambazo huweza kuathiri akili na tabia ya mtu. Mara nyingi watu hawa hujiingiza katika ulevi ambao huwa ni mgumu kuacha kutokana na hali ya kuuzoesha mwili kuishi na madawa haya kila siku.
Mfano wa dawa ya kulevya ni kama
Pombe
Heroin
Bangi
Kokeini
Tumbaku
Orodha ya dawa za kulevya za hospitali
Baadhi ya dawa ambazo hutolewa hospitali zinazoweza kuwa dawa za kulevya
Ambien
Amphetamines
Ativan
Barbiturates
Benzodiazepines
Carisoprodol
Clonazepam
Codeine
Concerta
Demerol
Desoxyn
Dexedrine
Dextroamphetamine
Dextromethorphan
Diazepam
Dilaudid
Gabapentin
Hydrocodone
Hydromorphone
Klonopin
Librium
Lorazepam
Methadone
Norco
Opioids
Opana
Oxycodone
Oxycontin
Painkillers
Percocet
Phenobarbital
Prescription Stimulants
Ritalin
Roxicodone
Soma
Suboxone
Subutex
Tramadol
Tussionex
Ultram
Valium
Vicodin
Vyvanse
Wellbutrin
Xanax
Zolpidem
Dalili za mtu anayetumia dawa ya kulevya
Kutanuka kwa pupil
Kupungua uzito kwa muda mfupi
Kutojijari kisafi
Matatizo ya meno
Kupata matatizo ya ngozi
Matatizo ya kupata usingizi
Kuwa mkali na msumbufu
Kuwa na hali ya msongo wa mawazo
Kuwa na hali ya huzuni
Kubadili tabia
Kuchoka
Kuwa na mambo ya utani mwingi
Kujihusisha na mambo mengi ya kiuhalifu
Dalili za uteja wa dawa za kulevya
Kujihisi kuwa unapaswa kutumia dawa hizo mara kwa mara
Kuwa na shauku kubwa ya kutumia dawa bila kuacha
Kutumia dawa kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya muda unaotaka wewe ikae mwilini
Kutumia hela kubwa kununua madawa hata kama huna uwezo nazo
Kuendelea kutumia dawa na huku unajua inasababisha matatizo mwilini
Kuweza hata kuiba dawa ili ujitosheleze
Kuendesha gari au kufanya shughuli zingine huku ukiwa kwenye athari za dawa bila kujua madhara yake
Kutengeneza namna ya ulaghai kupata dawa
Kujaribu kuacha huku unashindwa
Madhara ya kutumia dawa za kulevya
Kupata shida shuleni au masomoni
Mwanafunzi huyu huanza kushuka uwezo wake wa kimasomo kuanza kutokwenda darasani au kuchelewa kuingia darasani.
Kuathiriwa kiafya kwa kuishiwa nguvu na kushindwa kufanya shughuli zake za kila siku
Kutojijari
Mtu huyu huanza tabia za kujipuuza kwa kuwa mchafu na kutokuwa msafi
Kubadilika tabia
Mtu huyu huanza kuwa mkali na wa kuogofya kwa familia
Matumizi mabaya ya pesa
Mtu hutumia namna yoyote ile kupata madawa ya kulevya, mfano kutumia pesa zote anazozipata kununua dawa za kulevya.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 20:02:52
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.MayoClinic.DrugAddiction.https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/drug-addiction/symptoms-causes/syc-20365112. Imechukuliwa 17/4/2020
2.DrugAbuse.signsofsubstanceAbuse.https://drugabuse.com/symptoms-signs-drug-abuse-effects/. Imechukuliwa 17/4/2020
3.WebMb.SignsOfDrugAddictio.https://www.webmd.com/mental-health/addiction/signs-of-drug-addiction. Imechukuliwa 17/4/2020
4.Harrison Principles of Internal Medicine ISBN NI 9781259644030 Written by Tinsley R Harrison ukurasa wa 2562-2572