Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, MD
6 Desemba 2020, 16:54:56

Kuharisha kinyesi cheusi
Kuharisha hutokea endapo kinyesi hakichatengenezwa vema ndani ya utumbo, hii hutokea kama maji hayajafyonzwa kwa kiwango cha kutosha katika mfumo wa utumbo mpana na hivyo kusababisha kutoa kinyesi kilaini zaidi kwa jina la uharo. Sababu mbalimbali zinaweza kupelekea kuharisha (zisome katika makala ya kuharisha). Katika makala hii utajifunza sababu za kuharisha kinyesi chenye rangi nyeusi.
Ni salama kuharisha kinyesi cheusi?
Kuharisha kinyesi chenye rangi nyeusi huweza kusababishwa na sababu za hatari zinazotakiwa kugunduliwa na kupatiwa ufumbuzi mapema au kusababishwa na sababu za kawaida ambazo hupaswi kuwa na hofu nazo. Hivyo endapo unaharisha kinyesi cheusi ni vema kuwasiliana na daktari wako kwa uchunguzi wa kutambua kisababishi, na ikiwa unafahamu kisababisha baada ya kusoma makala hii huna haja ya kuwa na hofu kwani hali yako itarejea sawa baada ya kuepuka kisababishi.
Visababishi
Sababu zinazopelekea kuharisha kinyesi cheusi ni;
Kuvilia kwa damu ndani ndani ya tumbo au sehemu za mwanzo ya utumbo mwembamba- hii huweza kusababishwa na vidonda vya tumbo au madhaifu mengine katika kuta za mfumo juu wa chakula
Kutumia madini chuma mfano vidonge vya madini chuma au dawa za kuongeza damu zenye madini chuma
Kutumia dawa zenye madini risasi
Kula vyakula vya rangi ya bluu au nyeusi mfano furu n.k
Kunywa dawa za kienyeji zenye rangi ya bluu au nyeusi
Vihatarishi
Vihatarishi vya kuharisha kinyesi chenye damu ni;
Kuwa na magonjwa kwenye ini
Saratani ndani ya mfumo wa chakula
Kuchanika kwa mrija wa esophagus
Maambukizi kwenye tumbo
Ischemia kwenye utumbo
Vidonda vya tumbo
Kuvimba kwa mishipa ya damu ya esophagus(varices)
Matumizi ya muda mrefu wa dawa jamii ya NSAIDS kama aspirini, diclofenac n.k
Maelezo zaidi
Kusoma zaidi kuhusu kuharisha na matibabu ya nyumbani ingia kwenye makala ya kuharisha.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 19:54:47
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. What Are the Causes of Black Stool?. https://www.verywellhealth.com/causes-of-black-stool-1941711# . Imechukuliwa 4.12.2020
2. Why Are My Stools Black?. https://www.healthline.com/health/bloody-or-tarry-stools. Imechukuliwa 4.12.2020
3. Alarm Symptoms: A Cause for Alarm?. https://iffgd.org/symptoms-causes/alarm-symptoms.html. Imechukuliwa 4.12.2020
4. Bowel and Bladder Problems. https://www.cancer.org/treatment/treatments-and-side-effects/physical-side-effects/stool-or-urine-changes.html. Imechukuliwa 4.12.2020
5. Stool color: When to worry. https://www.mayoclinic.org/stool-color/expert-answers/faq-20058080. Imechukuliwa 4.12.2020