top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Peter A, MD

17 Aprili 2020 17:09:28

Maumivu ya pua
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Maumivu ya pua

Maumivu ya pua huweza kutokana na sababu mbalimbali, ni rahisi kwa pua kuumia na kupata maambukizi kutokana na kuwepo kwa matundu mawili ambayo hupitisha hewa pamoja na vimelea kama bakteria virusi na fangasi.


Visababishi


Baadhi ya visababishi vikuu ni


 • Ajali

 • Sinusaitizi (sinusitis)

 • Nazo fyuronkyurosisi

 • Sarkoidosisi

 • Kutoboka kwa septamu ya pua

 • Saratani


Ajali

Ajali ni moja ya sababu kuu ya maumivu ya pua, mara nyingi hutokea wakati wa michezo, kupigana ngumi, kuanguka au ajali ya vyombo vya moto.


Sinusaitizi

Ni hali ya kuvimba na maambukizi kwenye uwazi wa sainazi karibu na pua ,macho na chini ya mashavu ,mtu mwenye sinusaitizi huweza kuwa na dalili zifuatazo;


 • Kukohoa

 • Kuchoka

 • Homa

 • Maumivu ya kichwa

 • Kukosa uwezo wa kunusa- anozimia

 • Kutokwa na maji puani

 • Kuziba kwa pua


Nazo furonkurosisi

Ni maambukizi eneo la ndani la pua ambako kuna shina la nywele. Maambukizi huweza kuhama kutoka kwenye mfumo wa juu wa upumuaji na kuja puani au maambukizi ya bakteria mabo wapo kwenye pua. Vimelea vya kwenye pua vinaweza kusababisha maambukizi endapo kuta za pua zimeharibika kutokana na kuchokonoa pua au kuingia kwa kitu kigeni.


Dalili zingine ni kama


 • Pua kuwa na jalada kama kutu

 • Kuwa nyekundu

 • Kutoa harufu mbaya kwenye pua

 • Kuvimba


Sarkoidosisi

Ugonjwa huu husababisha dalili ya maumivu ya pua na kuziba, ugonjwa huu hutokea kwa mara chache, ukitokea husabababisha kuvimba kwa tishu za pua na kutengeneza uvimbe kwa ndani. Dalili zinazoambatana ni;


 • Kutokwa na damu puani

 • Kubadilika kwa rangi ndani ya pua

 • Anozimia (kushindwa kunusa)

 • Kuziba kwa pua

 • Kuvimba kwa pua


Kutoboka kwa septamu ya pua

Ni tundu ambalo huonekana katika sehemu ya mfupa unaotenganisha matundu mawili ya pua ,tundu hili husababisha maumivu ya pua na hupelekea kuonekana kwa dalili zingine kama hali ya ukutu kwenye pua, kuongezeka kwa shinikizo la damu la pua , Kuhema kwa shida na mlio wa filimbi unapohema


Saratani

Mara chache maumivu ya pua huweza kuashiria saratani kwenye pua au vyumba vya sainazi, uvimbe wa saratani huweza kutokea kwenye upande zote au upande mmoja wa pua. Baadhi ya dalili zingine ni;


 • Macho kuchomoza nje

 • Ganzi ya usoni

 • Maumivu ya kishwa

 • Kukosa uwezo wa kunusa

 • Kubana kwa pua

 • Pua kutoa damu

 • Kutokwa na usaha kwenye pua

 • Kutokuona vizuri

 • Kutokwa na uchafu kwenye macho

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 20:02:52

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

bottom of page