top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Mangwella S, MD

18 Juni 2021, 18:56:57

Maumivu ya tumbo na kifua wakati wa mazoezi
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Maumivu ya tumbo na kifua wakati wa mazoezi

Maumivu ya tumbo au maumivu chini ya kifua upande wa kulia wakati wa mazoezi ni aina ya maumivu yanayotokea wakati wa kufanya mazoezi na hupotea mara unapoacha kufanya mazoezi.


Maumivu hayo licha ya kutokea sana upande wa kulia, huweza tokea pia upande wa kushoto na hufahamika kwa jina jingine kama maumivu mpito ya mazoezi.


Kuacha, kupunguza ukali wa mzoezi, kupumzika au kujinyoosha mwili husadia kupunguza maumimu haya.


Katika makala hii, maumivu chini ya kifua upaned wa kulia wakati wa mazoezi, maumivu ya kifua upande wa kushoto wakati wa mazoezi au maumivu ya tumbo wakati wa mzoezi yameelezewa kwa jina moja la maumivu mpito ya mazoezi.


Sifa za maumivu mpito ya mazoezi


Maumivu mpito ya mazoezi yanaweza kuwa na sifa zifuatazo;


  • Maumivu ya kunyonga

  • Maumivu butu

  • Maumivu ya kuvuta

  • Maumivu makali

  • Maumivu ya kuchoma kama sindano

  • Kutokea wakati wa mazoezi ya muda mrefu kama kutembea, kukimbia, kuendesha baiskeli, kucheza mpira wa kikapu

  • Maumivu yanayohamia begani kwa mazoezi makali zaidi


Nini kinasababisha maumivu mpito ya mazoezi?


Tafiti hazijaweza sema kisabaishi halisi cha maumivu chini ya kifua au tumbo wakati wa mazoezi, hata hivyo baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa wakati wa mazoezi ogani ndani ya tumbo (ini, bandama na matumbo) zilizoshikwa na ligamenti kwenye ukuta wa dayaframu, unaotenga mapafu na matumbo huwa na mvutano mkubwa. Mvutano huu husababisha uchokozi na majeraha kidogo ambayo huleta dalili ya maumivu ya chini ya kifua au tumbo haswa upande wa kulia.


Bofya picha juu ya makala hii kuangalia uhusiano wa dayaframu na ogani ndani ya tumbo


Tafiti zingine pia kuwa wakati wa mazoezi kuna ongezeko la damu kwenye misuli ya ukuta wa dayaframu, ongezeko hili hupelekea hisia za maumivu ya chini ya kifua au tumbo wakati wa mazoezi.


Vihatarishi


Mambo au matendo yafuatayo yanaongeza hatari ya kupata maumivu mpito ya mazoezi;


  • Kula mlo mkubwa au kutumia vinywaji vyenye sukari nyingi muda mfupi kabla ya mazoezi

  • Kufanya zoezi kali au kwa muda mrefu zaidi

  • Kuwa mgeni kwenye mazoezi ( kutokuwa mzoefu wa mazoezi)


Namna ya kuzuia maumivu mpito ya mazoezi


Ili kuzuia maumivu chini ya kifua au tumbo wakati wa mazoezi fanya mambo yafuatayo;


  • Fanya zoezi mwili wako ukiwa umenyooka, epuka kukunja mgongo haswa wakati unatembea, kimbia au kucheza mpira wa kikapu

  • Usitumie vinywaji vyenye sukari kwa wingi muda mfupi kabla ya mazoezi

  • Usile mlo mkubwa wenye mafuta au nyuzinyuzi kwa wingi muda mfupi kabla ya kufanya mazoezi

  • Punguza ukali wa mazoezi unayofanya

  • Ongeza ukali wa mazoezi taratibu, kwa wiki au kila baada ya siku kadhaa ili mwili uzoee taratibu ongezeko hilo

  • Endapo unafanya mazoezi ya kutembea au kukimbia, ongeza umbali unaotembea taratibu kila wiki badala ya kuongeza umbali ghafla.

  • Wasiliana na daktari wa mazoezi kwa ushauri zaidi kuhusu maumivu endapo yanaendelea licha ya kufanya njia zilizoorodheshwa hapo juu


Namna ya kutibu maumivu mpito ya mazoezi


  • Endapo umeanza kupata maumivu, punguza ukali wa mazoezi, mfano kama unatembea, punguza hatua za kutembea na baada ya hapo ongeza taratibu mpaka pale ambapo hutahisi maumivu.

  • Vuta pumzi kwa kina kisha itoe taratibu kwa dakika kadhaa

  • Inua mkono mmoja uende nyuma ya kichwa upande unaosikia maumivu, kufanya hivi utanyoosha misuli ya tumbo. Unaweza fanya hivyo upande mmoja na kwenda mwingine.

  • Inamia taratibu upande ambao unapata maumivu.

  • Simama kisha shika sehemu inayouma kwa mkono wako kisha inamisha kiwiliwili kwenye upande wenye maumivu. Fanya hivi kwa dakika chache na unaweza kurudia rudia


Wakati gani utafute msaada wa daktari unapopata maumivu mpito ya mazoezi?


Kwa kawaida maumivu mpito ya tumbo au chini ya kifua wakati wa mazoezi hupotea yenyewe ndani ya dakika chache baada tu ya kuacha mazoezi. Endapo yatakuwa na sifa zifuatazo wasiliana na daktari haraka;


  • Kutoisha licha ya kuacha kufanya mazoezi

  • Kuambatana na dalili zingine kama kukohoa kushindwa kupumua au homa

  • Kuvimba upande unaopata muumivu


Je unapata vichomi tumboni na si maumivu ya mazoezi?


Endapo unapata vichomi tumboni, soma kuhusu makala hizo kwenye linki zinazofuata


Dalili za ugonjwa

Kichomo cha kifua


ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

8 Oktoba 2021, 04:53:21

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Morton D, et al. (2015). Exercise-related transient abdominal pain (ETAP). DOI:
10.1007/s40279-014-0245-z. Imechukuliwa 18.06.2021

2. Morton DP. (2003). Exercise related transient abdominal pain.
bjsm.bmj.com/content/37/4/287. Imechukuliwa 18.06.2021

3. Muir B. (2009). Exercise related transient abdominal pain: A case report and review of the literature.
ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2796944/. Imechukuliwa 18.06.2021

4. Dr. Brad Muir, et al. Exercise related transient abdominal pain: a case report and review of the literature. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2796944/. Imechukuliwa 18.06.2021

bottom of page