top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

14 Septemba 2023 17:13:09

Tumbo kujaa gesi na kuvuruga
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Tumbo kujaa gesi na kuvuruga

Dalili hii ya tumbo kujaa gesi mara nyingi husababishwa na ulaji wa vyakula vya  aina fulani, hata hivyo kuna baadhi ya matatizo ya kiafya yanayoweza kusababisha tatizo hili.

 

Ingawa watu wengi hufahamu kwamba tumbo kujaa gesi husababishwa  na kula maharagwe, ama vitunguu, ni muhimu kutambua kwamba kuna sababu zingine pia  ambazo zinajumuisha ulaji wa vyakula vilivyoorodheshwa hapa chini;

Vyakula vinavyosababisha tumbo kujaa gesi

 • Ulaji wa vyakula vyenye maziwa au maziwa

 • Matunda aina kadhaa yenye gesi kwa wingi kama vile tufaa, tikiti maji na peasi

 • Soda viazi vitamu na viazi mviringo

 • Mahindi ya kuchemsha au kuchoma

 • Pilau

Sukari aina ya fructose inayopatikana kwenye matunda na soda, lactose inayopatikana katika maziwa au vyakula vyenye mazao ya maziwa na vyakula vya kusindikwa huwa visababishi vikuu vingine vya tumbo kujaa gesi, maumivu ya tumbo, na kuhara

 

Dalili zingine zinazoweza kuambatana na tumbo kujaa gesi na kuvuruga ni;
 • Kuhisi mvurugiko wa tumbo

 • Kuhisi sauti za mijongeo ya tumbo

 • Kubeua mara kwa mara

 • Maumivu ya tumbo

Visababishi

Katika sehemu hii utajifunza visababishi vingine vya tumbo kujaa gesi mbali na vyakula ambacho ni kisababishi kikuu

Tatizo la tumbo kujaa gesi pia linaweza kusababishwa na magonjwa yafuatayo;

 
 1. Ugonjwa wa syndrome ya Irritable bowel

 

Ugonjwa huu hutokea kutokana na mvurugiko wa mfumo wa tumbo, huwa ni vigumu sana kugunduliwa na dakitari kwa sababu dalili zake hufanana na magonjwa mengine.

 

Dalili zifuatazo huweza kuambatana na ugonjwa huu;

 • Tumbo kujaa gesi

 • Kuvimba kwa tumbo

 • Kuhisi mvurugiko wa tumbo

 • Kukosa choo kwa muda wa wiki moja na kufuatiwa na kuhara wiki inyofuata

 

Hakuna kisababishi halisi kinachosababisha ugonjwa huu ila kuna vihatarishi vinavyofahamika vinachangia kuamsha tatizo hili kama vile

 • Kuharibika kwa mfumo wa vichochezi mwili

 • Kuharibika kwa mfumo wa fahamu wa ubongo

​​​

2. Kiungulia

3. Maambukizi ya giardia

4. Matumizi ya baadhi ya dawa

5. Kuongezeka uzito

6. Magonjwa ya akili kama msongo wa mawazo, shauku kuu na sononeko

7. Magonjwa ya kula kama anoreksia nevosa na bulimia nevosa

8. Mwili Kutohimili vyakula vya laktosi

Matibabu 

Matumbo ya mtu huwa hayana tatizo lolote na  mwathilika huwa mzima katika mfumo wa chakula, dalili za ugonjwa huu mara nyingi huwa mbaya wakati wa jioni. Cha kusikitisha ni kwamba hakuna tiba kwa ajili ya kuondoa kabisa tatizo hili, kinachofanyika ni kupunguza dalili na kubadili mfumo wa maisha tu.

 

Matibabu ya nyumbani
 • Punguza vyakula vya nyuzinyuzi zinazotokana na vyakula vya mbegu huweza kusaidia kupunguza dalili za tatizo hili kwa asilimia 20 hadi 30

 • Zuia kula mikate, mayai, ngano, biskuti , vitumbua, maandazi na vyakula vingine jamii ya ngano.

 • Zuia vyakula vingine kama mayai au vyakula vyenye mayai kwa sababu huleta gesi

 • Zuia  kula vitu vifuatavyo kama utaweza, ngano, vitunguu, kabeji, alizeti, maharagwe, tufaa,tikiti maji, peasi,

 • Zuia kutafuna bigijii ili kuepuka kumeza gesi

 • Tafuna chakula taratibu kuzuia kumeza gesi, pia usile mlo mkubwa kwa wakati mmoja

 • Zuia kumeza chakula na maji ili kuepuka gesi kuingia tumboni

 • Tumia vyakula visivyo na maziwa au mazao ya maziwa

 • Fanya masaji ya tumbo kukusaidia ubeue gesi iliyo tumboni

 • Tumia dawa za kusaidia mmeng'enyo wa vyakula vya laktozi na gluteni

 • Zuia kupata haja ngumu au kukosa haja kubwa kwa muda mrefu, tumia vyakula vya kulainisha tumbo na kunywa maji ya kutosha oamoja na kufanya mazoezi

 • Ongea na daktari wako kuhusu kutumia dawa za antibayotiki endapo gesi yako inasababishwa nabakteria kwenye tumbo

 • Tumia mafuta yenye minti (kuzuia) kupata gesi

 

Onana na daktari wako endapo umefanya matibabu ya nyumbani pasipo kupata  nafuu yoyote ndani ya wiki moja

Wakati gani uwasiliane na daktari unapokuwa na hali hii?

Mwone daktari wako endapo unapata dalili ya tumbo kujaa gesi pamoja na;

 • Maumivu makali ya tumbo na endelevu

 • Unapata damu kwenye choo, kupata choo cheusi au kinachonata kama lami

 • Unapata homa kali

 • Kuharisha

 • Kuzidi kwa kiungulia

 • Kutapika

 • Kupoteza uzito bila sababu

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

14 Septemba 2023 17:13:09

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

Thiwan S. (n.d.). Abdominal bloating: A mysterious symptom.
med.unc.edu/ibs/files/educational-gi-handouts/Abdominal%20Bloating.pdf. Imechukuliwa 29.06.2020

Wang TJ, et al. (2020). The effect of abdominal massage in reducing malignant ascites symptoms.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/25558030. Imechukuliwa 29.06.2020

Functional GI disorders. (2020). iffgd.org/functional-gi-disorders.html. Imechukuliwa 29.06.2020

Gas. (2018). my.clevelandclinic.org/health/diseases_conditions/hic_Gas. Imechukuliwa 29.06.2020

Mayo Clinic Staff. (2020). Bloating, belching and intestinal gas: How to avoid them.
mayoclinic.org/diseases-conditions/gas-and-gas-pains/in-depth/gas-and-gas-pains/art-20044739. Imechukuliwa 29.06.2020

Seo AY, et al. (2020). Abdominal bloating: Pathophysiology and treatment.
jnmjournal.org/journal/view.html?uid=327&vmd=Full. Imechukuliwa 29.06.2020

bottom of page