top of page

Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali

Unashauriwa kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Uono hafifu wa macho

Uono hafifu wa macho

Ni hali ya macho kupoteza nguvu ya kuona au ukosefu wa uwezo wa macho kuona vitu vema inavyoviangalia, hii inapelekea kushindwa kuona vema taarifa za kitu kinachoangaliwa na wengine huita 'kuona ukungu.

Kuziba ghafla njia ya juu ya mfumo wa hewa

Kuziba ghafla njia ya juu ya mfumo wa hewa

Kunaweza kuwa hatari kwa maisha, husababisha sauti ya strido wakati wa kuvuta hewa, kupumua kwa shida, na matumizi ya misuli ya ziada ya kupumua.

Mkojo mchafu

Mkojo mchafu

Mkojo mchafu imetumika kumaanisha neno tiba la 'urine Cloudiness'. Hii ni hali inayotokea endapo mkojo unatoka ukiwa na uchafu au ukiwa mzito na wenye uchafu mweupe tofauti na kawaida.

Kutokwa na damu ukeni kwenye komahedhi

Kutokwa na damu ukeni kwenye komahedhi

Kutokwa na damu baada ya komahedhi si jambo la kawaida na kunaweza kuwa ishara ya matatizo mbalimbali kuanzia ukavu wa uke hadi saratani ya mfuko wa uzazi. Mwanamke yeyote anayepata damu baada ya kuacha hedhi kwa miezi 12 mfululizo anapaswa kufanyiwa uchunguzi wa daktari mapema.

Vidonda kwenye ulimi

Vidonda kwenye ulimi

Vidonda kwenye ulimi ni vidonda vinavyotokea kwenye ulimi. Vidonda vya ulimi vinaweza kuwasha wakati wa kula chakula au kunywa kinywaji chenye chumvi chumvi.

bottom of page