Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali
Unashauriwa kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Dalili za upungufu wa damu
Upungufu wa damu mwilini kwa jina la kitiba Anemia humaanisha upungufu wa seli nyekundu za damu zinazoitwa hemoglobin. Kiwango cha kawaida cha chembe za damu za haemoglobin kweney mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa Kila mililita ya damu, kiwango pungufu ya Hapo mtu mtu husemekana kuwa ana tatizo la upungufu wa damu.

Dalili za tezi dume
Tezi dume kwa lugha ya tiba "Prosteti" ni tezi iliyo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume, chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi hii hupitiwa katikati na mrija wa urethra unaotokea kwenye kibofu cha mkojo kwenda kwenye tundu la uume. Mrija huu kazi yake ni kutoa mkojo kwenye kibofu cha mkojo.



