top of page

Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali

Unashauriwa kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Majeraha ya uti wa mgongo

Majeraha ya uti wa mgongo

Huathiri upumuaji kulingana na eneo lake, ambapo jeraha kati ya C3-C5 husababisha matumizi makubwa ya misuli ya ziada. Dalili ni Babinski’s rifleksi, misuli kukakama, kupoteza hisia, na sindromu Horner’s kwa majeraha ya seviksi ya chini.

Edema ya ghafla ya mapafu

Edema ya ghafla ya mapafu

Husababisha kupumua kwa shida, haraka na kwa ugumu kwenye pozi la kulala, miruzi na kikohozi chenye makohozi ya rangi waridi yenye povu. Wagonjwa pia huonyesha moyo kwenda kasi, wasiwasi, ngozi baridi na yenye ubluu.

Kuchuruzika udenda

Kuchuruzika udenda

Kutokwa na udenda ni ishara ya kushindwa kumeza mate inayotokana na kuferi kufanya kazi au kupooza kwa misuli ya uso au madhaifu ya mfumo wa fahamu inayoongoza ufanyaji kazi wa misuli ya usoni na mara chache sana kwa sababu ya matumizi ya dawa au sumu aina fulani zinazoongeza uzazlishaji wa mate katika kinywa.

Aneurismu ya Aota ya tumbo (Inayopasuka)

Aneurismu ya Aota ya tumbo (Inayopasuka)

Ni hali hatari inayosababisha maumivu makali ya tumbo la juu yanayosambaa hadi mgongo, pamoja na uvimbe unaodunda kabla ya kupasuka. Dalili za mshtuko kama mpwito wa moyo wa kasi, kupumua haraka, na ngozi baridi huonekana baada ya kupasuka.

Maumivu ya bandama

Maumivu ya bandama

Hujitokeza upande wa juu kushoto wa tumbo na kusambaa hadi bega la kushoto, yakizidi kwa kuvuta pumzi. Dalili zinaweza kujumuisha kukaza kwa tumbo na msuguano wa bandama.

bottom of page