Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic
Matibabu
Matibabu huhusisha
Kuongezewa maji kupitia mishipa ya damu au kunywa mpaka mwili utakapokuwa umetosheka. Maji haya yatasaidia kurudisha kiwango kilichopote wakati ulipokuwa unakojoa sana na kuzimua sukari katika damu
Kupata madini(electroliti)- electroliti ni madini katika mwili ambayo hubeba umeme katika mwili wako kama kalisium, sodium potassium na chloride. Madini haya huwa kwenye kiwango cha chini pale mwili unapokosa insulin. Hivyo utapokea electroliti kupitia mishipa ili kusaidia moyo misuli na mishipa ya fahamu kufanya kazi.
Homoni Insulin- insulin huondoa tatizo linalosababisha DKA, pamoja na matibabu ya electrolyte na maji utapewa homoni ya insulin kupitia mishipa ya damu. Kiwango cha sukari kikishuka na kufikia 13.3mmol/l au 240mg/dl dawa ya insulin kupitia mishipa itasimamishwa na utapewa kupitia sindano ya kuchoma kwenye mwili
Jinsi mwili utakapoitikia matibabu daktari atafanya vipimo vingine ili kuona nini kilichosababisha DKA na mara nyingi unaweza kuandikiwa dawa za kupambana na bakteria kama utakuwa na maambukizi y bakteria mwilini. Kama kushikwa kwa moyo kumesababisha DKA basi vipomo zaidi vya moyo vitaanyika. Kama ndo mara ya kwanza kutambuliwa na kisukari basi utapewa dalasi na taratibu wa kufanya kuhusu matibabu endelevu.
Imechapishwa 3/3/2015