top of page

Maana

​

Dalili

​

Visababishi

​

Vihatarishi

​

Madhara

​

Vipimo

​

Matibabu

​

Kujikinga

Visababishi

 

Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic

​

Sukari ni chanzo kikubwa cha nguvu katika seli za mwili, homoni ya insulin husaidia sukari kutumiwa na seli kwa kuiingiza ndani ya seli.

​

Bila insulin, mwili wako hauwezi tumia sukari kiusahihi, hivyo mwili huanza kutafuta nguvu kutoka kwenye vyanzo vingine kama mafuta. Mwili unapokuwa unavunja mafuta kwa ajili ya kujipatia nguvu kemikali asidi ya ketone huzalishwa. Kiwango cha ketone kinapozidi kwenye damu hupelekea kuonekana kwenye mkojo.

 

Tatizo la DKA huweza kuamshwa na

Magonjwa- maambukizi au magonjwa mengine yanaweza kuamsha mwili kuzalisha homoni kama adrenaline na cortisol. Homoni hizi hupinga kazi za insulin na huweza kupelekea kuamshwa kwa tatizo la DKA. Maambukizi ya nimonia na mfumo wa mkojo(UTI) husababisha mara kwa mara tatizo la DKA.

 

Matumizi ya insulin yasiyo sahihi- kama ukikosa dozi moja au unatumia insulin dozi ndogo inaweza pelekea kupungua kwa insulin katika damu na kuamsha DKA.

 

Visababishi vingine ni kama

  • Kupigwa au kuumizwa kihisia

  • Kushikwa kwa moyo

  • Madawa ya kulevya au pombe haswa madawa ya cocaine

  • Madawa aina ya corticosteroid na madawa na baadhi ya madawa ya kufanya ukojoe sana.

 

 

Imechapishwa 3/3/2015

bottom of page