Maambukizi ya kirusi cha ebola
​
Imeandaliwa na madaktari wa ULY-Clinic
Ebora ni moja kati ya virusi 30 vinavyoweza kusababisha homa ya kutokwa na damu. Genusi ya kirusi cha ebola kwa sasa bado kimegawanyika katika makundi matano ambayo ni:
-
Sudani Ebolavirus,
-
Zaire eboravirus,
-
taiforest(ivory coast) eboravirus,
-
Reston ebora virus na
-
bundibugyo Ebolavirus.
Mlipuko wa ugonjwa wa kirusi cha Ebolavirus mwaka 2014 huko afrika magharibi ilihusisha kirusi cha Zaire Ebolavirus, ulikuwa mlipuko mkubwa sana katika historia ya ugonjwa huu duniani.
Ni vema kuangalia magonjwa ya milipuko kabla hujaenda baadhi ya nchi ili kujua hali ya usalama katika nchi hizo nazoenda
Shirika la Chakula na madawa la Us food lilipitisha vipimo viwili vya haraka kwa ajili utambuzi wa kirusi huyu kwenye damu na mkojo kwa mda wa saa moja tu kwenye baadhi ya hospitali na kuzipa uwezo wa kupima kipimo hicho, pia kipimo cha pili ni kile ambacho damu au mkojo hupimwa kwenye maabara maalumu na majibu hutoka kati ya masaa 24 hadi 48
Imechapishwa 3/3/2016
Imeboreshwa 5/11/2018