Virusi hawa hutunzwa wapi?
Imeandaliwa na madaktari wa ULY-Clinic
Utafiti ulifanyika katika miaka ya 1966 huko DRC kongo na kirusi cha ebola kimeonekana kwa wanyama aina 19 na mimea aina 24. Virusi vya ebola vimeonekana katika matunda yanayoliwa na popo pamoja na popo wenyewe na hujizalia kwenye popo na matunda hayo pasipo kufa.
Kwa jinsi gani husafilishwa.
Virusi vya ebola vya afrika husafilishwa kutoka kwa mtunzaji asiyejulikana (labda popo) kwenda kwa binadamu au mmea na mnyama asiye binadamu. Sana sana kwa kupitia majimaji na damu kutoka kwenye ngozi laini, macho mate na matumbo kwa kupitia michaniko midogo sana katika ngozi na kwa vipimo vya kitaalamu kumeonyesha hata kwa njia ya hewa pia kunaeneza ugonjwa huu.
Mwbwa nao wameonekana kuambukizwa virusi hivi pasipo kuonyesga dalili yoyote, maambukizi haya hutoka katikakinyesi, mkojo au damu kutoka kwa mtunzaji(host) asiyefahamika.
Mlipuko wa mara ya kwanza wa kirusi cha ebora uliolipatiwa ni ule wa mwaka 1976 huko yambuku, DRC kongo ambapo watu 316 waliambukizwa. Kundi jingine la mlipuko ulifanyika mwaka 1995 ambapo watu 318 waliathiriwa na ugonjwa huu. Kukosa kwa vifaa vya kujikinga na kirusi huyu kwa wataalamu wa afya wakiwa kazini, wakati wa kuwahudumia wagonjwa hawa kulichangia kusambaa kwa ugonjwa huu kwa watu kwa sababu maambukizi yalikuwa yanaenezwa kwa vifaa vya kazi hasa sindano na kuliongeza uenezaji wa ugonjwa wa ebola hospitalini.
imechapishwa 3/3/2016
Imeboreshwa 5/11/2018