top of page

Elimu ya magonjwa kwa mjamzito

Sehemu hii utajifunza maelezo ya ziada kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa ujauzito. Unashauriwa siku zote kuwasilaina na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile iliyoandikwa humu ili kupata ushauri unaoendana na hali yako ya kiafya.

Levocetirizine na ujauzito

Levocetirizine na ujauzito

Hakuna ripoti zinazoelezea matumizi ya levocetirizine kwa binadamu mjamzito. Taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo kwa hatari kiasi, na hivyo kufanya kutowezekana kufahamu kuhusu madhara kwa ya kiuumbaji kwa kichanga. Hakuna taarifa zinazosema kwamba dawa jamii ya antihistamine pamoja na hii ni sumu ambayo inaweza pelekea kutokea kwa madhara ya kiuumbaji kwa kichanga tumboni. Licha ya hayo, endapo matumizi ya antihistamine yatahitajika wakati wa ujauzito, uchaguzi ni kutumia dawa zenye taarifa na zinappnekana kuwa afadhali zaidi kama vile chlorpheniramine au diphenhydramine.

Ticarcillin-clavulanic acid  kwa ujauzito

Ticarcillin-clavulanic acid kwa ujauzito

Tafiti nyingi zimeonyesha kutokuwepo kwa madhara kwa kijusi na mtoto anayezaliwa na mama aliyetumia dawa hii.

Daptomycin na ujauzito

Daptomycin na ujauzito

Kuna ripoti tatu zinaelezea matumizi ya daptomycin kwenye kipindi cha pili na tatu cha ujauzito. Tafiti za uzazi kwa wanyama zinaonyesha kuweko kwa hatari kidogo, lakini hakuna taariza za kutosha kutoka kwa binadamu hivyo kuzuia kufanya uchuguzi wa madhara ya dawa hii kwa kichanga tumboni.Hata hivyo antibiotic nyingi zenye uzito mkubwa huwekwa kwenye kundi la hatari kidogo kwenye ujauzito, hivyo isisitishwe kwa sababu ya ujauzito.

Telbivudine na ujauzito

Telbivudine na ujauzito

Kuna taarifa chache kuhusiana na matumizi ya dawa hii kwa binadamu wajawazito. Ingawa taarifa za wanyama wajawazito zinatia moyo, taarifa za binadamu wajawazito zinatakiwa kupatikana ili kutoa hitimisho kuhusu usalama wake kwenye ujauzito wa binadamu.

Gentamicin na ujauzito

Gentamicin na ujauzito

Gentamicin hutumika sana kwenye matibabu ya magonjwa kwa mama mjamzito.Uhusiano wa dawa hii na kutokea kwa madhaifu ya kiuumbaji hayajaonekana bado licha ya kutumika sana

bottom of page