top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. PEter R, CO

Dkt. Benjamin L, MD

Jumapili, 27 Machi 2022

Pilipili hoho
Pilipili hoho

Pilipili Hoho ni tunda lilopatikana kwenye kundi la mbogamboga kutoka kwenye familia ya Solanaceae, mbali na kuongeza ladha kwenye chakula, pilipili hoho inafaida nyingi kwa miili yetu hiyo ni kutokana na uwepo wa virutubisho na madini kwa ukuaji wa afya za mwanadamu.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Pilipili Hoho


 • Mafuta

 • Madini

 • Sukari

 • Nyuzilishe

 • Protini

 • Vitamini

 • Kabohaidreti

 • Maji

Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Pilipili Hoho


Kwenye pilipili Hoho kuna Kemikali Muhimu ziitwazo Capsaicin na Ascorbic Acid


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Pilipili Hoho yenye gramu 100


 • Nishati = 20kcal

 • Mafuta = 0.2g

 • Maji = 93.89g

 • Kabohaidreti = 4.6g

 • Sukari = 2.4g

 • Nyuzilishe = 1.7g

 • Protini = 0.9g


Vitamini zinazopatikana kwenye Pilipili Hoho yenye gramu 100


 • Vitamini A = 18mcg

 • Vitamini B1 = 0.057mg

 • Vitamini B2 = 0.028mg

 • Vitamini B3 = 0.480mg

 • Viatmini B5 = 0.99mg

 • Vitamini B6 = 0.224mg

 • Vitamini B9 = 10mcg

 • Vitamini C = 80mg

 • Vitamini E =0.37mg

 • Vitamini K = 7.4mg


Madini yanayopatikana kwenye Pilipili Hoho yenye gramu 100


 • Kalishiamu = 10mg

 • Kopa = 0.07mg

 • Floraidi = 2mcg

 • Madini Chuma = 0.34mg

 • Magineziamu = 10mg

 • Manganaizi = 0.122mg

 • Fosifolasi = 20mg

 • Potashiamu = 175mg

 • Sodiamu = 3mg

 • Zinki = 0.13mg


Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Pilipili Hoho


 • Kupunguza maumivu yatokanayo na magonjwa ya muda mrefu mfano maumivu yatokanayo na saratani

 • Husaidia kutibu vidonda vya tumbo, ugonjwa wa kuharisha , kikohozi, vidonda vya koo pamoja na meno.

 • Huimarisha mfumo wa damu na hivyo kupunguza athari za kupatwa na ugonjwa wa moyo

 • Hushusha sukari na kuweka msawazo wa sukari mwilini pamoja na kuzuia ugonjwa wa kisukari

 • Kuimarisha kinga ya mwili, kusaidia kuongeza hamu ya kula

 • Huimarisha na kuifanya ngozi ing`ae

 • Hupunguza changamoto zitokanazo na ukomo wa hedhi kwa wanawake

Imeboreshwa,
14 Mei 2022 22:11:19
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Peppers. https://www.nutritionvalue.org/Peppers%2C_raw%2C_green%2C_sweet_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 10 January 2022.

 2. Dutta A, Deshpande SB. Mechanisms underlying the hypertensive response induced by capsaicin. Int J Cardiol. 2010 Nov 19;145(2):358-359. doi: 10.1016/j.ijcard.2010.02.034. Epub 2010 Mar 11. PMID: 20223533. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/20223533/. Imechukuliwa tarehe 10 January 2022.

 3. Maji AK, Banerji P. Phytochemistry and gastrointestinal benefits of the medicinal spice Capsicum annuum L.(Chilli):a review. J Complement Integr Med. 2016;13:97–122. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6000222/. Imechukuliwa tarehe 10 January 2022.

bottom of page