Habari za afya
Soma habari mpya na matukio katika fani za afya kutoka kona mbalimbali za Dunia na Tanzania

Programu ya Mafunzo ya Uandaaji wa Lishe Bora ya Mtoto
Ni muhimu kuchagua nafaka zisizokobolewa, mikunde yenye protini nyingi na mbegu zenye mafuta mazuri kama karanga na mbegu za maboga wakati wa kuandaa unga wa lishe ya mtoto. Malighafi zinapaswa kuwa safi, bila ukungu au wadudu, na ni vyema kuchanganya vyakula vinavyopatikana kirahisi ili mtoto apate virutubishi kamili.

Boresha Afya yako na Jamii kwa kushiriki Utafiti
Jiunge na ULYCLINIC kushiriki katika utafiti wa Jukwaa la Afya la Akili unde kwa Kiswahili na uchangie kuboresha uelewa wa afya kwa wagonjwa na wahudumu wa afya. Ushiriki wako wa hiari utasaidia kuimarisha huduma za afya na kuchochea maendeleo ya kisayansi kwa kutumia lugha yetu ya Taifa, Kiswahili.

Dawa Mpya zinazobadilisha Matibabu ya Magonjwa Makuu 2025–2026
Donidalorsen, Plozasiran, Aficamten, Elamipretide, na Ziftomenib (Komzifti) ni dawa mpya za tiba ya uvimbe wa mwili wa kurithi, matatizo ya mafuta mengi kwenye damu, ugonjwa wa kutanuka kwa moyo, ugonjwa wa nishati ya seli, na saratani kali ya damu aina ya mayeloidi leukemia. Ugunduzi wa dawa hizi ni hatua muhimu katika tiba ya kisasa inayolenga sababu za msingi za ugonjwa badala ya dalili tu.

Tahadhari ya Magonjwa ya Milipuko: Influenza, UVIKO-19, Dengue na Kipindupindu
Kwa mujibu wa taarifa ya Mganga Mkuu wa Serikali ya tarehe 25/02/2026, Wizara ya Afya imeonya kuhusu hatari ya kuongezeka kwa maambukizi ya Influenza, UVIKO-19, Dengue na Kipindupindu, hasa katika kipindi cha mvua na mabadiliko ya hali ya hewa. Wananchi wameshauriwa kuzingatia usafi binafsi na wa mazingira, kudhibiti mazalia ya mbu, kutumia maji salama, na kuwahi hospitalini mapema ili kuzuia kusambaa kwa magonjwa haya.

Tofauti ya AI na Daktari katika kutafsiri maswali
AI hutegemea uandishi ulio wazi na mantiki iliyopangwa ili kutafsiri swali, hivyo maswali yasiyoeleweka hupunguza usahihi wa majibu. Daktari, kwa upande mwingine, hutumia uzoefu, muktadha, na hisia za kitaalamu kutafsiri hata maswali yasiyo rasmi na kutoa majibu sahihi zaidi.
