Huduma ya kwanza
Katika sehemu hii utajifunza kuhusu huduma ya kwanza kwenye matukio mbalimbali ili uweze kuwa msaada pale itakapohitajika kabla wataalamu wa afya hawajafika kwenye tukio

Degedege kwa mtoto: Huduma ya kwanza
Degedege kwa mtoto mdogo huitwa kwa jina la kitiba kama seizure, fits au convulsion, hii hutokana maranyingi na kuongezeka kwa joto la mwili linalohusiana na maambukizi ya koo, masikio, malaria, na maambukizi mengine ya maradhi kwenye mwili wa mtoto. Hata hivyo sababu zingine zinaweza kuwa ni kupungua kwa sukari mwilini

Mshiko wa pumu ya kifua-Asthma: Huduma ya kwanza
Mtu mwenye mshiko wa pumu msaidie akae katika mkao wa kupumua vizuri, atumie dawa yake ya kupulizia aliyoandikiwa, mtulize na mfuatilie kupumua na fahamu, huku ukiondoa kichochezi ikiwa kinaonekana.
Piga 112 haraka ikiwa dalili ni kali, dawa haisaidii, hawezi kuzungumza vizuri, anachoka sana, midomo inakuwa bluu/kijivu au anapoteza fahamu, kwa kuwa mshiko mkali wa pumu unaweza kutishia maisha.

Kushikwa ghafla na hofu na kupumua haraka haraka: Huduma ya kwanza
Mtu hushikwa na hofu kubwa ya ghafla endapo endapo alikuwa na shauku kuu, hofu hii huambatana na dalili za kimwili ambazo ni kupumua haraka haraka, kutokwa na jasho, mapigo ya moyo kwenda harakaharaka au kuruka na kukakamaa kwa misuli

