top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeandikwa:

Dkt. Mangwella S, MD

Dkt Salome A, MD

3 Julai 2023 15:44:10

Cifran CT

Cifran CT ni jina la kibiashara la dawa ya antibayotiki. Kidonge cha Cifran CT ni muunganiko wa dawa mbili zinzotumika katika matibabu ya maambukizi ya vimelea kwenye mfumo wa uzazi, meno, njia ya mkojo, mapafu na tumbo.


Dawa hii hufanya kazi kwa kuua bakteria gramu hasi, chanya na protozoa wanaodhuriwa na dawa tu na inashauriwa kutumika kama ilivyoelekezwa na daktari wako.


Naweza tumia Cifran CT na chakula?

Cifran CT inapaswa kutumika pamoja na chakula kwa dozi na wakati uliopangiwa na daktari ili iweze kufanya kazi vema.


Usitumie zaidi ya dozi uliyoshauriwa na daktari wako kwa kuwa dawa inaweza kuleta madhara mwilini endapo utazidisha kiwango. endapo umesahau kunywa, kunywa mara utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi inayofuata umekaribia sana.


Maudhi ya dawa

Baadhi ya maudhi ya dawa hii ni;

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Maumivu ya tumbo

  • Kukosa hamu ya kula

  • Maumivu ya kichwa n.k


Unawezaje kuepuka maudhi kiasi

Ili kuepuka madhara haya inashauriwa kula mlo kamili na kunywa maji ya kutosha wakati unatumia dawa hii


Maudhi makubwa ya dawa(madhara ya dawa)

Kama maudhi ya dawa yamekuwa makubwa, unapaswa kuwasiliana na daktari wako mara moja kwa ushauri na tiba. Dalili hizo zinaweza kuwa;

  • Harara kwenye ngozi

  • Muwasho wa mwili

  • Kuvimba

  • Kuishiwa pumzi

  • n.k


Naweza kutumia Cifran CT kaitika ujauzito?

Kwa sababu dawa hii ni mchanganyiko wa dawa mbili, ili kufahamu unaweza kutumia au la unapaswa kufahamu kila dawa inashauriwaje kuhusu matumizi yake kwa mjamzito. Soma zaidi kwa kubofya katika makala zianzofuata.

Uly clinic inakushauri siku zote wasiliana na daktari wako kwa ushauri wa matumizi ya dawa yoyote. Usitumie dawa bila kushauriwa na daktari ili kuepuka madhara na kufanya vimelea kuwa sugu kwenye dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia linki ya 'Pata tiba' au 'Wasiliana nasi' chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii:

  1. Cifran CT Tablet. https://www.1mg.com/drugs/cifran-ct-tablet. Imechukuliwa 03.07.2023

  2. Cifran CT Tablet. https://www.apollopharmacy.in/medicine/cifran-ct-tablet. Imechukuliwa 03.07.2023

  3. Tinidazole kwa mjamzito. ULY CLINIC.https://www.ulyclinic.com/madhara-ya-dawa-kwa-mjamzito-na-mto/tinidazole-na-ujauzito. Imechukuliwa 03.07.2023

Imeboreshwa:

3 Julai 2023 20:22:32

bottom of page