Pen V ni jina la kibiashara la dawa inayofahamika kama Penicillin V, moja ya antibayotiki kundi la penicillin inayotibu magonjwa yanayosababishwa na bakteria wanaodhuriwa na dawa hii kama vile magonjwa ya koo, masikio, ngozi na kinga ya homa ya moyo.