top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:28:14
Damu mbichi kwenye kinyesi (himatokizia)
Majina mengine: haematochezia, rectal bleeding (Kiingereza)
Aina ya neno: dalili
Maana: kutoa damu mbichi kwa njia ya haja kubwa.
Maelezo zaidi
Visababishi: bawasiri, mpasuko wa njia ya haja kubwa, kuhara damu (shigella, amiba), kichocho cha utumbo, kolaitisi ya vidonda, vinyama, saratani ya utumbo mpana au puru.
Damu nyingi sana huweza kutoka juu (tumbo) ikipita haraka.
Kwa mtu zaidi ya miaka 40, damu kwenye kinyesi ichunguzwe – usidhani ni bawasiri tu.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Damu nyingi, kizunguzungu au kuzirai, homa na kuharisha damu, kupungua uzito, au mabadiliko ya choo yanayodumu.
Tazama pia: Kinyesi cheusi (melina), Mpasuko wa njia ya haja kubwa (anal fissure)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 17:28:03
bottom of page

