top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:28:14

Kinyesi cheusi (melina)

Kinyesi cheusi (melina)

Majina mengine: melaena (Kiingereza)


Aina ya neno: dalili


Maana: kinyesi cheusi chenye damu iliyomeng'enywa.


Maelezo zaidi


  • Visababishi: vidonda vya tumbo (hasa kwa wanaotumia dawa za maumivu za NSAIDs au aspirini), mishipa iliyovimba ya umio kwa wenye ugonjwa wa ini, saratani ya tumbo.

  • Vidonge vya madini chuma na baadhi ya vyakula (mf. vyenye rangi nyeusi) hufanya kinyesi kuwa cheusi lakini kigumu na bila harufu ya lami – si damu.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Kinyesi cheusi kama lami, hasa pamoja na kizunguzungu, kuzirai au kutapika damu – ni dharura.


Tazama pia: Mishipa iliyovimba (varices), Damu mbichi kwenye kinyesi (himatokizia)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 17:28:03

bottom of page