top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:28:14

Mishipa iliyovimba (varices)

Mishipa iliyovimba (varices)

Majina mengine: vena zilizovimba; varicose veins, oesophageal varices (Kiingereza)


Aina ya neno: hali ya ugonjwa


Maana: vena zilizotanuka kupita kiasi.


Maelezo zaidi


  • Umio na tumbo: ini kusinyaa (cirrhosis) na kichocho cha ini ndio visababishi vikuu Tanzania; hutapika damu nyingi ghafla – dharura.

  • Miguuni: kusimama muda mrefu, ujauzito, unene, kurithi; husaidiwa na soksi za kubana na kunyanyua miguu.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Kutapika damu au kinyesi cheusi kwa mwenye ugonjwa wa ini – ni dharura.


Tazama pia: Ini kusinyaa na kuwa na makovu (cirrhosis), Kinyesi cheusi (melina)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 17:28:03

bottom of page