top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:11:16

Mapigo ya moyo kwenda haraka (takikadia)

Mapigo ya moyo kwenda haraka (takikadia)

Majina mengine: takikadia; moyo kwenda kasi; moyo kwenda mbio; kasi kubwa ya mapigo ya moyo; tachycardia (Kiingereza)


Aina ya neno: dalili / kiashiria


Maana: moyo kupiga zaidi ya mara 100 kwa dakika kwa mtu mzima aliyepumzika. Kwa kawaida mapigo ya moyo ya mtu mzima aliyepumzika ni 60–100 kwa dakika; kwa watoto kiwango cha kawaida ni cha juu zaidi kulingana na umri.


Maelezo zaidi


  • Ya kawaida (mwitikio wa mwili): mazoezi, hofu, maumivu, homa, kahawa au chai nyingi.

  • Kutokana na ugonjwa: upungufu wa maji mwilini, kutokwa na damu, upungufu wa damu, tezi ya thyroid kufanya kazi kupita kiasi, maambukizi makali, baadhi ya dawa, au hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo.

  • Mara nyingi huambatana na mpapatiko wa moyo (palipitesheni), kizunguzungu au kuchoka haraka.


Lini umwone mtaalamu wa afya haraka


  • Maumivu ya kifua, kupumua kwa shida, kuzirai au kuchanganyikiwa.

  • Mapigo yanazidi 150 kwa dakika ukiwa umepumzika, au yanaanza na kuisha ghafla mara kwa mara.

  • Una ugonjwa wa moyo unaojulikana.


Tazama pia: Moyo kwenda kasi; Kuhisi mapigo ya moyo; Mpapatiko wa moyo (palipitesheni)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page