top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:11:16

Ugonjwa wa seliaki (coeliac disease)

Ugonjwa wa seliaki (coeliac disease)

Majina mengine: celiac disease, coeliac disease, gluten enteropathy (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa


Maana: uharibifu wa vinyweleo vya utumbo mdogo unaochochewa na gluteni kwa watu wenye vinasaba vya hatari.


Maelezo zaidi


  • Dalili: kuharisha kwa muda mrefu, kinyesi chenye mafuta na harufu, tumbo kuvimba, uchovu, upungufu wa madini chuma usiopona, kwa watoto kutokua vizuri; wengine hupata upele wenye mwasho (dermatitis herpetiformis).

  • Hutambuliwa kwa vipimo vya damu vya kingamwili na kipande cha utumbo mdogo – mgonjwa aendelee kula gluteni mpaka vipimo vifanyike.

  • Matibabu: kuepuka gluteni maisha yote; vyakula salama ni pamoja na mahindi, mchele, mtama, uwele, muhogo, viazi, ndizi, maharage.

  • Hutofautiana na mzio wa ngano au kutostahimili lactose.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Kuharisha au tumbo kujaa kunakodumu, kupungua uzito, au upungufu wa damu usioeleweka – pima.


Tazama pia: Kuharisha (diarrhoea), Magonjwa ya kinga kushambulia mwili (autoimmune diseases)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page