top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:28:15
Virutubishi vidogo (micronutrients)
Majina mengine: micronutrients (Kiingereza); vitamini na madini
Aina ya neno: neno la lishe
Maana: virutubishi vinavyohitajika kwa miligramu au mikrogramu.
Maelezo zaidi
Upungufu wa kawaida Tanzania: madini chuma (upungufu wa damu), vitamini A (upofu wa usiku, kinga dhaifu), iodini (goita, akili kudumaa), zinki, foliki asidi (kasoro za uti wa mgongo kwa watoto).
Njia za kupata: mlo mchanganyiko (mboga za majani, matunda, maharage, samaki, mayai, nyama), vyakula vilivyoongezewa virutubishi, nyongeza (vitamini A kwa watoto kila miezi 6, madini chuma na foliki asidi kwa wajawazito).
Tazama pia: Chumvi yenye madini joto (iodized salt), Nyuzinyuzi (dietary fibre)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 17:28:03
bottom of page

