top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Bakteremia (Bacteremia) ni nini?

Bakteremia

Bakteremia ni uwepo wa bakteria kwenye mkondo wa damu, hali ambayo inaweza kuwa ya muda mfupi au kuendelea na kusababisha sepsisi kwa baadhi ya wagonjwa. Hutambuliwa kwa kipimo cha kuotesha damu na hutibiwa kulingana na chanzo cha maambukizi na aina ya bakteria waliobainika.

Mshituko wa sepsisi

Mshituko wa sepsisi

Mshituko wa sepsisi ni hatua kali ya sepsisi ambapo shinikizo la damu hushuka sana na viungo muhimu vya mwili hupata damu ya kutosha kwa shida. Ni dharura ya kitabibu inayohitaji matibabu ya haraka ili kuokoa maisha.

Sepsisi (Sepsis) ni nini?

Sepsisi

Sepsisi ni hali hatari inayotokea pale mwitikio wa mwili dhidi ya maambukizi unapoharibu viungo muhimu na kuhatarisha maisha. Hutokea kutokana na maambukizi mbalimbali na huhitaji utambuzi na matibabu ya haraka ili kuzuia madhara makubwa au kifo.

Vipele ni nini?

Vipele ni nini?

Upele ni uvimbe mdogo, mgumu, usio na maji, ulioinuka juu ya ngozi, na ni mojawapo ya alama muhimu katika uchunguzi wa magonjwa ya ngozi. Upele hufahamika kwa majina mengine kama vipele, mapele, kipele, uvimbe chini ya sentimita 1 juu ya usawa wa ngozi n.k.

QID kirefu chake ni nini?

QID kitiba ni kifupi cha neno la Kilatini "quater in die" lenye maana ya 'mara nne kwa siku'. Hutumika kwenye cheti cha dawa kumaanisha 'dawa itumike mara nne kwa siku' (ndani ya masaa 24) yaani dawa itumike kila baada ya masaa 6.

bottom of page